0
 KADA wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Mwigulu Nchemba,ameendelea kuchanja mbunga mikoani kusaka wadhamini ili kutimiza maelekezo na kanuni za chama hicho katika kutafuta nafasi ya kuteuliwa ndani ya chama kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu.
 Akiwa mkoani Rukwa,Mwigulu ameendelea kutoa kauli yake ya kukommesha kufanya kazi kwa mazoea katika maeneo mbalimbali kwa kuwa ni moja ya sehemu yenye matatizo na kupelekea kukwamisha mipango mbalimbali
 Mwigulu alisema anaimani na nafasi aliyoiomba katika kuwatumikia watanzania na kuahidi kuleta mabadiliko na mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa watanzania kwa kutumia rasiliamali zilizopo na kupunguza uwiano wa walionacho na wasio nacho
 Kada huyo wa CCM ambaye amekuwa akipata wadhamini wa kutosha kila mkoa aliokuwa akifika,amewaomba watanzania kuzidisha maombi ili vikao vya uteuzi vitakavyokaa viweze kuliona jina lake na kulipitisha

Post a Comment