0

Nawashukuru Wana-CCM,Watanzania wote popote mlipo,Nimezunguka Nchi nzima kutafuta wadhamini kwa kufuata taratibu na kanuni za Chama,Nimepata wadhamini Mikoa yote ya Tanzania,Naomba kuwashukuru sana kwa kuendelea kuniamini na Kunituma nikasimamie AGENDA ya Watanzania.

Sehemu kubwa ya nilikozunguka,Watanzania wameonesha imani kubwa juu yangu,Hivyo ahadi yangu kubwa kwa wote wenye Matumaini na wasio na Matumaini "NITAWAVUSHA".


Nimedhamiria kusimamia Uchumi wa Taifa letu kwenda kipato cha kati,Kupambana na tatizo la Rushwa,Kupambana na tatizo la Ajira nahitaji kuona watu wanafanya kazi kwa Shift Usiku na Mchana.,Kuboresha huduma za Jamii,Kufufua na kuanzisha Viwanda mbalimbali (ili vijana wapate ajira,Kupunguza wimbi za kuingiza bidhaa kutoka nje).


Watumishi wa Umma watoe huduma kwa wakati na kwa haki,Hakuna soko la haki za watanzania kwenye serikali ya awamu ya Tano.


Nahitaji kuona Mgawanyo sawa wa keki ya Taifa.
Nawaomba Watanzania,Mniunge mkono,Mniamini,NITAWAVUSHA.


Hii leo nimekabidhi fomu za wadhamini kama chama kilivyoagiza,Naamini hakuna anayeweza kushindana na AGENDA ya Watanzania.

Kidumu chama cha Mapinduzi
Mungu Ibariki Tanzania


 

Post a Comment