0

WATU watatu  wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kumuua mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Tabu Makanya na kukimbia na kichwa chake mkazi wa Kijiji cha  kwibara kata ya Mugango wilaya ya Butiama Mkoani Mara .


Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza na Jaji  Joakin Demola, aliyesikiliza kesi hiyo akiwa na  jopo  la Wanasheria  wapatao saba(7) kati ya hao walikuwepo wanasheria  watatu (3) waliokuwa  wakiwatetea washitakiwa hao .

 

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni  Ndaro Sumuni,Aberd Kazimili na Fidelisi Ngewa wote wakazi wa Kijiji cha  Kwibara kata ya Mugango wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara,huku Diwani wa Kata hiyo Wandwi Maguru aliachiwa na  Mkurugenzi wa mashita nchini.


Mtuhumiwa mwingine Mahakama ilisitisha kushikiliza kesi yake kutokana na  kuhisiwa kuwa na matatizo ya akili na amwingine wa tatu hajakamatwa hadi leo ambapo jumla walikuwa watuhumiwa sita .


Kabla ya hukumu hiyo  illiyotolewa  majira ya saa 4:30 asubuhi  Jaji huyo alielezea  tukio la mauji hayo na kusema  watuhumiwa katika kesi hiyo walienda  nyumbani kwa Diwani wa Kata hiyo  aitwaye Wandwi Maguru  ambapo  walikubaliana nae ili wampelekee kichwa hicho kwa makubaliano ya shilingi Milioni. 1.5.


Alisema makubaliano hayo ilikuwa kwamba baada ya kupelekewa kichwa hicho  diwani huyo angekifanyia mazindiko  ya uvuvi  wa samaki ambapo kikao chao cha makubaliano hayo kilifanyika nyumbani kwa Diwani huyo  Desemba 19 mwaka 2012 na watu hao walifanikiwa kutekeleza mauaji hayo baada ya siku mbili Desemba 21, 2012 majira ya usiku

 

Aliendelea kukumbushia zaidi kuwa kuuawa kwa mwanamke huyo Mahakamu Kuu imeelezwa  watuhumiwa watano walivamia nyumbani kwa Tabu Makanya ambaye kwa sasa ni marehemu kisha kumshambulia kwa siraha mbalimbali  yakiwemo marungu hatimaye kumchinja shingo lake  na kumtenganisha na kiwili wili  chake.


Aidha baada ya watuhumiwa hao kutimiza adhima yao   walichukua kichwa hicho na kukiweka ndani ya  gunia kisha kutoweka nacho  ambapo wananchi walipiga yowe  wakakitupa    chini kichwa  kilichookotwa na wanakijiji.


Zaidi ya wanawake 20 waliuawa katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2014 kutokana na imani za kishirikina na kesi kadhaa zilifikishwa mahamani nyingine kuhukumiwa na nyingine bado zinaendelea.

Post a Comment