0


HUDUMA YA BURE YA MADAKTARI BINGWA MJINI MUSOMA
NDUGU WANANCHI WA MKOA WA MARA,MNATANGAZIWA HUDUMA YA BURE YA UCHUNGUZI WA AFYA INAYOENESHWA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI PAMOJA NA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO CHINI YA MUUNGANO WA ASASI ZINAZO HUSIKA NA MAGONJWA YASIYOKUA YA KUAMBUKIZA(NCD).

MAGONJWA MBALIMBALI YANAFANYIWA UCHUNGUZI NA KUTOLEWA USHAURI UNAOFAA YAKIWEMO MAGONJWA YA MOYO,KISUKARI,SARATANI AINA ZOTE,MFUMO WA HEWA(PRESHA)FIGO,AFYA YA AKILI,AFYA YA KINYWA NA MENO PAMOJA NA MAGONJWA MENGINE YASIYOKUWA YA KUAMBUKIZA NA UPIMAJI WA VVU KWA WALE WANAOHITAJI.

HUDUMA HII INATOLEWA KWA SIKU MBILI ZA JUMAMOSI NA JUMAPILI TAREHE 1 NA 2 MWEZI AGOSTI KWENYE HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 12 JIONI,HIVYO WANANCHI WOTE MNAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATA HUDUMA HII MUHIMU KWAAJILI YA AFYA.

IMETOLWA NA DR.TATIZO
 WAANE,MWENYEKITI WA (TANCDA) NA DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO KUTOKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

 HUDUMA YA UPIMAJI WA UZITO NA UREFU PIA INATOLWA

 WANANCHI WAKISUBILI KUWAONA MADAKTARI
 MWANDISHI WA CHANEL TEN AUGUSTINE MGENDI NAYE ALIJITOKEZA KUPIMA
 DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO KUTOKA MUHIMBILI,DR.TATIZO WAANE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU HUDUMA ZINAZOTOLEA
 MWANDISHI WA TBC EMANUEL HAMAS NAE ALIJITOKEZA
 DICK HUNGA PRESHA ILIKUWA JUU,MPIGA PICHA ZA TELEVISHEN


Post a Comment