0

 

 AKIZUNGUMZA NA BLOG HII,MATHAYO ALISEMA BADO ANAYO CHACHU YA KUENDELEA KULETA MABADILIKO KWENYE JIMBO LA MUSOMA MJINI KAMA ALIVYOFANYA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2005-2010 KWANI BAADA YA HAPO MAMBO MENGI YAMESIMAMA YA KIMAENDELEO NA NI YEYE PEKEE AMBAYE ANAWEZA KUENDELEZA PALE ALIPOISHIA AKIWA MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI.
 
MATHAYO AMBAYE ALIPATA NAFASI YA KUHUDHULIA MIKUTANO 2 YA KAMPENI HUKU MINGINE AKIWAKILISHWA NA MMOJA WA WANA CCM,ALISEMA KUTOKANA NA MATATIZO YA KIFAMILIA ALISHINDWA KUHUDHURIA MIKUTANO MINGINE LAKINI YUKO PAMOJA NA WANACHAMA WENZAKE NA DHAMIRA YAKE BADO IKO PALEPALE NA KIKUBWA NI KUHAKIKISHA WAKAZI WA MUSOMA WANAONDOKANA NA UMASIKINI KWA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWEKE KIUCHUMI ILI KUONDOKANA NA HALI DUNI ZA MAISHA.
KURA ZA MAONI ZA UBUNGE NA UDIWANI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI ZINATARAJIWA KUPIGWA KESHO ILI KUWEZA KUPATA WAWAKILISHI WANAOTOKANA NA CHAMA HICHO


Post a Comment