0


Uongozi wa MRPC, uliomba msaada kutoka mfuko huo ili kufanikisha mkutano mkuu wa chama hicho pamoja na masuala mbalimbali ambapo PSPF imetoa kiasi hicho cha fedha ili kuweza kusaidia katika yale yaliyokusudiwa.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu,Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Mara,Sudi Hamza,alisema wamekuwa wakishirikiana katika mambo mbalimbali na vilabu vya Waandishi wa Habari hapa nchini na kudai msaada huo utasaidia katika sehemu ya kufanikisha.

Alisema msaada huo sio mwisho katika kusaidia masuala ya Waandishi wa Habari hususani katika kukutana na wadau na kuweza kuzungumzia masuala ya maendeleo ambayo kupatikana kwake kutasaidia jamii kubwa.

Akipokea msaada huo,mMakamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mko wa Mara,Shomari Binda,ameushukuru mfuko huo kwa msaada walioutoa kwaajili ya kusaidia mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo
Post a Comment