Baraza
la habari Tanzania (MCT) limeanza kutoa mafunzo maalumu wa waandishi
wa habari yatakayowajengea uwezo wa kuandika habari sahihi
zinazohusiana na masuala ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi
OCTOBA zitakazowapa wananchi uwezo wa kuwapima wagombea na hatimaye
kuchagua viongozi wenye sifa.
Hayo yamesemwa na ALAKOK MAYOMBO, afisa program mwandamizi wa
MCT anayesghulikia masuala ya viwango na ubora wakati akielezea
madhumuni ya mafunzo hayo yanayowashirikisha waandishi wa mikoa ya
MWANZA, GEITA, SIMIYU, KAGERA na SHINYANGA yatakayochukau siku TANO.
Kwa upande wake mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, CHRIZOSTOM
RWEYEMAMU katika ufunguzi wa mafunzo hayo amewahimiza waandishi wa
habari kuandika habari zenye ukweli ili wajiepushe ma dhara ambayo
wanaweza kukumbana nayo.,
Mafunzo hayo yamegawanywa katika mikoa iliyoko kwenye kanda SABA
ambapo jumla ya waandishi MIA MOJA SABINI na TANO hapa nchini
watanufaika na mafunzo hayo.
Post a Comment
0 comments