0
WANAMICHEZO wanaoshiriki michezo mbalimbali,wameshauriliwa kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara ili kujiepusha na maradhi ambayo yanaweza kuwatokea wawapo mchezoni ama baada ya michezo.

Ushauri huo ulitolewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara,Elias Godfrey,wakati akishiriki zoezi la kupima afya za wachezaji wa klabu ya Biashara United,lililofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini hapa.

Alisema suala la kuangalia afya kwa mchezaji ni kitu muhimu kabla na baada ya kushiriki michezo na kudai kufanya hivyo unakuwa umejiepusha na hatari ambayo inaweza kujitokeza ukiwa kwenye mchezo husika.

Elias alisema kila mchezaji anapaswa kuzingatia suala la kuangalia afya yake na sio vizuri kushiriki michezo kwa muda mrefu bila kutenga muda wa kufanya vipimo na kujua maendeleo ya afya.

"Niwashukuru sana uongozi wa klabu ya Biashara ambayo imeamua kutenga muda wa kuangalia afya za wachezaji na hili ni jambo kubwa ambalo linapaswa kuungwa mkono na kila mmoja.

"Tumewahi kuwashuhudia baadhi ya wachezaji wakipata matatizo na wengine wakipoteza maisha wakiwa mchezoni hivyo ni muhimu kuwa na utaratibu wa kupima afya kwa kila mchezaji na ni vyema viongozi wa klabu nyingine wakawa na utamaduni huu",alisema Elias.

Mganga huyo ambaye alikuwa akishirikiana na wataalamu mbalimbali wa afya  kupima na kutoa ushauri kwa wachezaji hao,alisema ni vyema kila mchezaji aliyeshiriki zoezi hilo kuzingatia ushauri waliopewa baada ya kufanyiwa vipimo.

Mwenyekiti wa klabu ya Biashara United,Selemani Mataso,alisema kwa kujua umuhimu wa kuangalia afya kwa wachezaji,waliamua kujipanga na kufanya zoezi hilo huku akidi litakuwa endelevu kwenye klabu hiyo na kutoa wito kwa klabu nyingine kuwa na utaratibu wa kuangalia afya za wachezaji.




LUZUNDANA AKIPATA USHAURI WA DOCTA BAADA YA VIPIMO

GEORGE AKIFATILIA MAELEZO YA DOCTA


KATOGORO HAKUWA NYUMA KUANGALIA AFYA
SHOMMI B BLOG PIA NI MMOJA WAO
SHUKU MMOJA WA MCHEZAJI KIONGOZI WA TIMU YA BIASHARA

FOLENI KWAAJILI YA VIPIMO


Post a Comment