0

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini,na Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo,ametoa vitabu elfu 20 vya masomo mbalimbali kwa shule za msingi na sekondari katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu mashuleni.

Sehemu ya vitabu vilivyotolewa ni pamoja na masomo ya hesabu na sayansi huku Mbunge akikisisitiza iwapo suala la elimu litaboreshwa watapatikana wasomi ambao watakuja kutumiwa na taifa katika kuinua uchumi.

Akizungumza na wawakilishi wa walimu wa shule 20 za sekondari na 10 za msingi katika makabidhiano ya voitabu hivyo yaliyofanyika kwenye shule ya sekondari Mkirira,Muhongo alisema kwa kutambua umuhimu wa elimu na kusoma vitabu,ameanza kutekeleza ahadi zake kwa kutilia mkazo elimu.

Alisema vitabu hivyo vitatumiwa vizuri na wanafunzi na kupata usimamizi mzuri kutoka kwa walimu,itakuwa ni faida kubwa katika kuinua kiwangop cha elimu na kuwafanya wanafunzi wengi wengi kufaulu masomo yao.

Muhongo alisema kwa kutambua umuhimu wa masomo ya sayansi,katika vitabu hivyo vimewekwa vitabu vya masomo hayo pamoja na hisabati ili kuwasaidia wanafnzi wanaosoma masomo ya sayansi kupata kujifnza vitu vingi zaidi.

"Leo nimekuja jimboni kwaajili ya kugawa vitabu kwa shule za sekondari na msingi ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kuinua kiwango cha elimu mashuleni na kutengeneza kizazi cha wasomi watakaokuja kusaidia taifa letu.

"Elimu haina mbadala na taifa lolote lililofanikiwa miongoini mwa mataifa mnayoyajua walianza mapema kuwekeza kwenye elimu na leo hii wanao wasomi wengi na sisi lazima tuwekeze kwenye elimu ya vijana wetu,"alisema Muhongo.

Katika changamoto za walimu wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi,Waziri Muhongo alisema tayari wameanza mipango madhubuti ya kuwapata walimu wa masomo hayo na kutaka ushirikiano uwepo kutoka kwa viongozi wote wa Jimbo la Musoma Vijijini ili kutengeneza miundombinu ya kuwapokea walimu hao.

Baadhi ya walimu na wanafunzi waliopokea vitabu hivyo,wamemshukuru Waziri Muhongo kwa kuwasaidia vitabu hivyo ambavyo vitasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza kiwango cha elimu kwa wanafunzi.
Post a Comment