0

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI,PROFESA SOSPETER MUHONGO,AMEINGIA SIKU YA  PILI YA KUKUTANA NA WANANCHI WANAOZUNGUKA MGODI WA ACACIA NORTH MARA NA KUENDELEA KUSISITIZA ADHIMA YAKE YA KUMALIZA MIGOGORO NA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZILIZOKUWA ZIKIJITOKEZA BAINA YA WANANCHI WANAOZUNGUKA MGODI HUO NA WAMILIKI WA MGODI. 

 KATIKA MIKUTANO ILIYOFANYIKA SIKU YA LEO,WANANCHI WAMEENDELEA KULALAMIKIA FIDIA NDOGO YA MAENEO YAO BAADA YA KUFANYIWA TATHIMINI NA KUMUOMBA WAZIRI HUYO KUTIMIZA ADHIMA YAKE KWA KUHAKIKISHA MAMBO YOTE YANAMALIZWA VIZURI ILI KUSIWEPO NA MIGOGORO MINGINE.

 MWANASHERIA WA MGODI WA ACACIA NORTH MARA AKIMUONYESHA WAZIRI MUHONGO MAENEO AMBAYO ANADAI WANANCHI WAMETEGESHA NYUMBA ILI WALIPWE ZIADA
 WANANCHI WAKIENDELEA KUTOA MALALAMIKO YAO HUKU MMOJA AKIONYESHA  CHEKI YA SHILINGI ELFU SABINI ALIYOANDIKIWA NA MGODI BADALA YA SHILINGI MILIONI SABA
 WAZIRI MUHONGO AKISISITIZA JAMBO HUKU KATIKATI YAKE AKIWEPO MBUNGE WA JIMBO LA TARIME VIJIJINI JOHN HECHE

 VIONGOZI MBALIMBALI WAKIMSIKILIZA WAZIRI MUHONGO ILI KUTATUA KWA PAMOJA MATATIZO YA NYAMONGO

 VIONGOZI WA MGODI WKIFATILIA MAELEZO YA WAZIRI AMBAPO ALIUNDA KAMATI AMBAYO HAIKUWAHUSISHA VIONGOZI WA WILAYA YA TARIME ILI KUFATILIA MATATIZO YA NYAMONGO


 WANANCHI WAKIENDELEA KUTOA MAELEZO YA MATATIZO YAO


 MBONGE HECHE(KULIA)AKITETA JAMBO NA MWENYEKITI WA HALIMASHAURI YA TARIME KATIKA MKUTANO WA WAZIRI
 
HECHE AKIZUNGUMZA KUHUSIANA NA MALALAMIKO YA WANANCHIPost a Comment