2
 MBUNGE WA JIMBO LA TARIME VIJIJINI,JOHN HECHE(CHADEMA),AMEMSIFIA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI,PROFESA SOSPETER MUHONGO,KWA KUTEKELEZA AHADI YAKE KWA  WAKATI KWA KUFIKA KWENYE JIMBO HILO MARA BAADA YA KUMALIZIKA VIKAO VYA KWANZA VYA BUNGE LA 11 ILI KUWEZA KUTATUA CHANGAMOTO MBAMBALI ZINAZOWAKABILI WANANCHI WANAOZUNGUKA MGODI WA ACACIA NORTH MARA.

AKIZUNGUMZA NA BLOG HII MARA BAADA YA KUMALIZA SIKU YA KWANZA YA ZIARA YAKE YA SIKU 4 KATIKA MAENEO YA VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MGODI HUO,HECHE AMESEMA WAZIRI HUYO ANAPASWA KUSHUKULIWA KWA HATUA ZA MAPEMA ALIZOZICHUKUA KWA KUWA ZIMEONYESHA NIA THABITI YA KUTAKA KUMALIZA MATATIZO YALIYOPO KWENYE MAENEO HAYO.


AMESEMA KATIKA SWALI LAKE ALILOULIZA BUNGENI KUHUSIANA NA CHANGAMOTO ZIKIWEMO FIDIA KWA WANANCHI WANAOZUNGUKA MGODI HUO,WAZIRI HUYO ALIMJIBU NA KUTOA AHADI YA KUONGOZANA NAE KUTEMBELEA MAENEO HAYO NA SASA TAYARI AMESHAKAMILISHA AHADI HIYO NA ANAAMINI ATAFANIKIWA KUFIKIA LENGO LAKE ALILOWEKA LA KUMALIZA MATATIZO KWENYE MAENEO HAYO.


KWA KUANZA KUTATUA MATATIZO HAYO,WAZIRI MUHONGO AMEANZA KUKUTANA LEO NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO ZAO KABLA YA KUKUTANA NA UONGOZI WA MGODI PAMOJA VIONGOZI WA SERIKALI NGAZI YA WILAYA ILI KUONDOA MATATIZO YALIYOPO

WAZIRI MUHONGO AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WANAOZUNGUKA MGODI WA NYAMONGO

 MBUNGE HECHE AKICHANGIA JAMBO
 WANANCHI WAKIZUNGUMZA KERO ZAO

 WANANCHI WAKIMSIKILIZA WAZIRI MUHONGO
 WAZIRI MUHONGO AKIMSISITIZIA JAMBO MENEJA WA MGODI WA ACACIA NORTH MARA,GARY CHAPMAN KATIKA KUONDOA CHANGAMOTO ZILIZOPO

 WAZIRI MUHONGO ALIPOTEMBELEA MAENEO YENYE MATATIZO KATI YA MGODI NA WANANCHI
 MBUNGE HECHE AKIMSISITIZIA JAMBO WAZIRI AWEZE KUTATUA

Post a Comment

Kwa nini unaandika kwa kutumia herufi kubwa? Unajua kuwa hiyo ni sawa na kupayuka na kubwatuka? Sasa unampayukia nani katika kiblog chako hichi? Ulishawahi kuona popote mtu akiandika kwa herufi kubwa tupu kama siyo Mbongo asiyeelewa lolote kuhusu mambo ya uandishi kama wewe hapo? UNATIA AIBU!!!