0
 DIWANI WA KATA YA IRINGO NA MDAU MKUBWA WA MICHEZO,JUMA HAMIS(IGWEE),AMEWASHAURI WAAMUZI WA SOKA MKOANI MARA KUTENDA HAKI NA KUACHA KUZIBEBA TIMU WAKATI WA MICHEZO YA LIGI YA MKOA ITAKAYOANZA HIVI KARIBUNI KWA KUZISHIRIKISHA TIMU KUTOKA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA MARA.
 

IGWEE AMETOA KAULI HIYO WAKATI AKIFUNGUA SEMINA YA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA LIGI HIYO ILIYOANDALIWA NA CHAMA CHA WAAMUZI MKOA WA MARA(FRAT)INAYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA SHULE YA MSINGI MKENDO.

ALISEMA KILA MWAMUZI AZINGATIE KANUNI WAKATI AKICHEZESHA MCHEZO NA KUSITOKEE TABIA YA KUIBEBA TIMU YOYOTE KWA KUSHAWISHIWA NA VIONGOZI AU MTU YOYOTE KWA LENGO LA KUIBEBA TIMU.


KATIKA KUTATUA BAADHI YA CHANGAMOTO ZA WAAMUZI,IGWEE AMEHAIDI KUTOA VIFAA KWA WAAMUZI WA WILAYA ZOTE ZIKIWEWE JEZI PAMOJA NA KUTOA KIASI CHA SHILINGI LAKI 6 ILI KUWASAIDIA WAAMUZI KATIKA SUALA LA NAULI ZA KUFIKA KWENYE VITUO.

 KATIBU WA FRAT,ARON MBEHO AKITOA NENO LA UTANGULIZI
 MWENYEKITI WA FRAT,RUHUMBIKA AKIZUNGUMZA NA WAAMUZI WA SOKA KABLA YA KUMKARIBISHA MGENI RASMI

 MMOJA WA WAAMUZI AKICHANGIA JAMBO
 DIWANI IGWEE AKIFUNGUA SEMINA YA WAAMUZI WA SOKA MKOA WA MARA CHINI MHESHIMIWA IGWEE AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAAMUZI NA VIONGOZI WA FRAT

Post a Comment