0


SIKU moja baada ya kufikia tamati ya wiki ya Sheria,wananchi wa Manispaa ya Musoma,wamesema tatizo kubwa ambalo wanaliona ni kutokuwepo kwa Mahakama kuu mkoani Mara.

Kutokana na huduma za Mahakama kuu kupatakana jijini Mwanza,wananchi hao walidai wanatumia gharama kubwa kufatilia kesi zinazosikilizwa huko na wakati mwingine kesi hizo zikichukua muda mrefu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na BLOG hii, walisema  ni vyema serikali ikafanya jitihada za haraka kuhakikisha huduma hiyo inapatikana Musoma.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Wambura Mataso,alisema kwa kipindi cha miaka 6 amekuwa akifanya safari kwenda mkoani Mwanza kufatilia kesi yake na hadi sasa bado kesi hiyo haijamalizika na haijulikani itamalizika lini.

Alisema serikali ya awamu ya tano katika kuwapunguzia majukumu wananchi wake,ni vyema ikaangaliwa na huduma ya Mahakama kuu Musoma ambayo itatumiwa na wilaya zote za mkoani  Mara katika kuwaletea huduma karibu.

"Kwa kweli kwenye eneo hili tumekuwa tukipata tabu sana ya kufuata huduma ya Mahakama kuu jiji Mwanza na kutumia fedha nyingi ambazo zingeweza kusaidia katika majukumu mengine ya kifamilia,"alisema Mataso.

Mkurugenzi wa shirika la msaada wa kisheria kwa makundi maalum ya kijamii(LSAC),Ostack Mligo,alisema licha ya changamoto hiyo ya huduma ya Mahakama kuu,lakini wananchi wengi wanahitaji msaada wa kisheria.

Alisema shirika lake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa shughuli za kisheria ikiwemo Mahakama,wameamua kutenga muda wa kutoa elimu kwa wananchi ili wajue baadhi ya taratibu za kisheria maana wengine hawajui hata namna ya ufunguaji wa kesi kutokana na shida zao.

Mligo alisema kwa muda wa siku nne wananchi watembelee kwenye mabanda ya utoaji elimu ya kisheria ili waweze kupata msaada ambao unatolewa bure na wanasheria mbalimbali wanaoshiriki shughuli hiyo.

Wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo,Mkuu wa Wilaya ya Musoma,Zelothe Stephin,alisema ni vyema watumishi wa Mahakama wakafanya huduma bora kwa wananchi kutokana na malalamiko juu yao na kuacha kujihusisha na vitendo vya Rushwa.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 Wanasheria na Mahakimu wakiwa kwenye maandamano

 askari wakiongoza maandamano




 Mgeni rasmi akipokea maandamano

 Mshehereshaji Hakimu Maganga akitoa maelekezo
 Wananchi wakifatilia maadhimisho ya wiki ya Sheria
 Ustadh Rashid akisoma dua
 Padri kutoka Kanisa Katoriki akishiriki maadhimisho hayo kwa kusoma dua

Mkuu wa Wilaya ya Musoma,Zelothe Stephine,akisoma hotuba
 Mawakili wakifatilia maadhimisho
 Dalali wa Mahakama,Dommy Othumani Juma(kushoto)akifatilia
 Mahakimu wakifatilia


 Mwanasheria wa Serikali mkoa wa Mara akisoma hotuba






Post a Comment