|
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kapten mstafu, Aseri Msangi,
amewataka wananchi kuondokana na imani potofu kuwa upulizwaji wa dawa ya
ukoko majumbani mwao kwa ajili ya kinga dhidi ya Malaria huchangia
kupoteza nguvu za kiume.
Msangi ameyasema hayo juzi wakati
akizindua zoezi la unyunyiziaji wa dawa ya koko lililofanyika katika
wilaya ya Butiama ambapo zoezi hilo litafanyika katika wilaya za
Butiama na Musoma vijijini kuanzia machi 9 hadi April 22 mwaka huu
ambapo jumla ya majengo 47,577 kwa Wilaya ya Butiama na 31,824 kwa
Musoma vijijini zinatarajia kupulizia dawa ya ukoka.
Amesema
imani potofu zimekuwa zikichangia kwa kiwango kikubwa kuzorotesha zoezi
hilo na kuwataka wanannchi kutoamini hivyo badala yake wawe tayari
kushirikiana na wahusika pindi watakapokuwa wakiwafikia katika kaya zao.
Msangi
amesema ugonjwa wa malaria mkoani Mara umekuwa tishio kwa asilimia 25
kutokana na taarifa ya utafiti wa viashiria vya Malaria na Ukimwi
ulioendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kudai juhudi zaidi
zinapaswa zifanyike kati ya wananchi na taasisi mbalimbali ili kufikia
kiwango cha kitaifa cha kupunguza malaria ambacho ni asilimia 9.
Hata
hivyo amefafanua kuwa ugonjwa huo bado unaongoza kwa wagonjwa wengi
wanaolazwa katika vituo vya afya na zahanati kwa nchi 10 za kusini mwa
Afrika ikiwemo Tanzania ambapo nchi hizo zimekuwa zikichangia
takiribani asilimia 70 kwa ukubwa wa ugonjwa huo duniani.
Amesema
kutokana na utafiti ina maana kwamba mtu mmoja anapoteza maisha kwa
kila dakika moja kutokana na ugonjwa huo na kwa mwaka 2012 iliua watoto
takiribani 482,000 wa umri chini ya miaka mitano na kudai ni jukumu la
kila mmoja kutokomeza ugonjwa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa shirika lisilo la kiserikali la Abt Associates la Marekani ambao
wanasaidia kutokomeza Malaria nchini Tanzania na Afrika kwa Ujumla,Dk.
Nduka Uwuchukwu, amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na
Tanzania katika kuhakikisha ugonjwa huo unapungua na kupunguza vifo
vinavyotokana na ugonjwa huo.
Amesema jukumu la kupambana na
Malaria ni la kila mmoja na ni muhimu kuhakikisha kila kaya
inanyunyuziwa dawa ya ukoko ili kuteketeza mazalia yote ya mbu waenezao
Malaria katika wilaya za Butiama na Musoma vijijini. |
MKUU WA MKOA AKIPOKELEWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA VIWANJA VYA OFISI YA HALIMASHAURI YA BUTIAMA
TIMU YA WANYUNYUZIAJI
MKUU WA MKOA AKITETA JAMBO NA DK.NDUKA ANAYEONGOZA TIMU YA WANYUNYUZIAJI KAMA M KURUGENZI WA SHIRIKA LA Abt
MKURUGENZI WA Abt AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI
MKUU WA MKOA AKIELEKEA KUZINDUA
AKIPATA MAELEKEZO KABLA YA UZINDUZI
AKIJIANDAA KUZINDUA
BAADAE MAELEKEZO YALITOLEWA NYUMBA ZOTE ZINYUNYUZIWE
Post a Comment
0 comments