1

MBUNGE wa Jimbo la Musoma vijijini na Waziri wa Nishati na Madini,Profesa,Sospeter Muhongo,amekabidhi gari la wagonjwa kwenye kituo cha afya cha Murangi ili kuweza kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa huduma huku wananchi wa Jimbo hilo wakishukuru msaada huo.


 Akikabidhi gari hilo lililotolewa kwa msaada wa serikali ya Japan,Waziri Muhongo alisema anatambua changamoto mbalimbali zinazopatikana katika huduma za afya hivyo atajitahidi kufanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na marafiki zake ili kuweza kuzitatua.

Alisema gari ambalo amelikabidhi linazo huduma zote za kimatibabu ambazo mgonjwa ataweza kuzipata akiwa ndani ya gari kabla ya kufikishwa anakopelekwa kwaajili ya matibabu zaidi.

Muhongo alisema ni wajibu wa kila mmoja kulitunza gari hilo huku akiwataka wananchi kuwa walinzi wa kwanza kuhaakikisha linadumu na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi za kimatibabu pale zinapohitajika huduma za kupelekwa kwenye hospitali za rufaa. "Ndugu zangu gari hili na la kisasasa na ndani ya gari kuna vifaa vyote vinavyohitajika kumsaidia mgonjwa ikiwemo hewa ya oksjeni itakayoweza kumsaidia mgongwa kupumua wakati akipelekwa kwenye matibabu zaidi.

"Nimeambiwa na daktari aliyelifanyia ukaguzi gari hili kuwa hapa nchini gari zenye huduma kama hizi zipo mbili moja hospitali ya taifa ya Muhimbili na mmoja ndio hii mliolipata wananchi wa Jimbo la Musoma vijijini hivyo lazima muone umuhimu wake na kulitunza,"alisema profesa Muhongo.

Alisema licha ya wananchi kupata gari hilo,marafiki zake kutoka nchini China wamesaidia kutoa madawa mbalimbali ambayo yatatolewa bure kwa wananchi wenye magonjwa pamoja na madaktari bingwa 6 kutoka nchini humo kutoa huduma ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa bila malipo kwa muda wa siku 2.

Awali akitoa maelezo kuhusu huduma za afya zinazotolewa kwenye hospitali hiyo na Jimbo zima la Musoma vijijini,Mganga wa Wilaya ya Musoma,Genchwele Makenge,alisema bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ocheleweshwaji wa dawa kutoka (MSD) na upungufu wa watoa huduma.

Alisema msaada ambao umetolewa na Mbunge kuhakikisha upatikanaji wa gari pamoja na madawa utasaidia kuboresha huduma za afya na kuahidi kusimamia utunzwaji wa gari na kutumia madawa yaliyotolewa kwa lengo lililokusudiwa.

 Hapa Muhongo akifurahi akiwa ndani ya gari hilo
 Hapa akikabidhi nyaraka za gari na ufunguo kwa uongozi wa wilaya na kituo hicho cha afya
 Akiongea na Mganga wa kituo ndani ya gari
 Wananchi wakipita ndani ya gari

Post a Comment

Safi sana na mungu ambaliki sana nimatumaini yetu sasa wakazi wa musoma vijijin watapata huduma kwa halaka zaid tofauti na hapo awali mpaka gari litoke musoma mjini kwenda kumchukua mgonjwa hususani wamama wajawazito sasa vifo vya mama na mtoto vitaisha ubarikiwe sana mhe. Mbunge Pro. Mhongo mungu akubariki sana.