0
 MABINGWA wa soka mkoa wa Mara timu ya Igwe SC,leo imechomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa kutoka mkoa wa Simiyu timu ya Ambassador FC,katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Vijana mjini Muleba na kufikisha pointi 4 baada ya mchezo wa awali kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Mashujaa kutoka mkoa wa Kigoma.

Baada ya matokeo hayo,kocha wa timu ya Igwe,Sospeter Charles maarufu kwa jina la Big Sos,amesema vijana wake wamemsikiliza na kucheza kwa kujituma na kupata matokeo hayo na amewahakikishia mashabiki wa soka hususani wa mkoa wa Mara kupata matokeo katika mechi zijazo na kuendelea kuwaombea dua

 Kabla ya game kuanza muhimu kusalimiana
 Mambo ya Fail Pray
 Dua ni muhimu kabla ya mchezo kuanza
 Kikosi kilichoanza kuinyamazisha Simiyu
 Mapumziko Igwe ilitoka ikiongoza 1
 Baadae kocha ni kutoa maelekezo zaidi
 Majeruhi nao walipata nafasi ya kutibiwa
 Msisitizo

Post a Comment