0


 MKUU wa mkoa wa Mara,Magesa Mulongo,jana alilazimika kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyantwali hadi majira ya saa 2 usiku huku taa ya chemli ikitumika kumulikia mkutano ili aweze kusikiliza kero mbalimbali za wananchi alipokuwa kwenye ziara ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais kuwa mkuu wa mkoa huo.

Katika mkutano huo ulioanza majira ya saa 10 jioni baada ya kiongozi huyo kufanya mikutano mingine kwenye vijiji vya Kisangwa,Mcharo  na Ligamba,mkuu huyo wa mkoa alisema kutokana na kuonekana Kijiji hicho kina kero nyingi atalazimika kuwasikiliza wananchi hata usiku ukiingia ili apate kujua matatizo yao.


Kutokana na kuibuka kwa malalamiko mengi ya wananchi kwenye mkutano huo juu ya viongozi wa serikali ya Kijiji ikiwemo kushindwa kusoma kwa mapato na matumizi tangu mwaka 2014,alilazimika kutoa amri kwa jeshi la polisi kuwaweka chini ya ulinzi Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti ili waeleze yale yanayoendelea kwenye Kijiji hicho...........



 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda akimmulikia mkuu wa mkoa ili kusoma taarifa aliyoiomba kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Bunda juu ya mgogoro wa mtu aliyedaiwa kuwa gerezani na kukuta nyumba yake imeuzwa na mke wake kisha kukimbia
 Taa ya chemli iliyokuwa ikimulika mkutano huo

 Huu ulikuwa ni mkutano wa awali uliofanyika Kijiji cha Mcharo
 Hapa alitembelea shamba darasa la zao la muhongo kwenye Kijiji cha Kung'ombe
 Wananchi wakifatilia mikutano ya RC Mulongo wilayani Bunda
 Mwananchi akitoa kero zambe ya mkuu wa mkoa


Mkuu wa mkoa akifatilia kwa makini kero za wananchi



Post a Comment