0
 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt,John Pombe Magufuli,amewataka viongozi wa halimashauri,manispaa na majiji kuacha kutoa kazi kwa wakandarasi wazembe na wasiomaliza kazi wanazopewa kuzifanya.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa,George Simbachawene,kwenye ufunguzi wa mkutano wa 32 wa Jumuiya ya Seikali za Mitaa Tanzania(ALAT) ilidai kila kiongozi atimize wajibu wake kwa kuzisimamia kazi zote.

Amesema viongozi wa halimashauri wanao wajibu mkubwa katika kusimamia majukumu mbalimbali ya serikali za mitaa na kudai wapo wakandarasi ambao wanapewa kazi na kushindwa kuzifanya kwa mujibu wa mikataba na kutaka kila kiongozi kuzuia hali hiyo.

Katiba hutuba hiyo iliyogusa maeneo mbalimbali ya usimamizi wa shughuli za halimashauri,manispaa na majiji iligusia pia masuala ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo ndiyo chanzo muhimu cha mapato kwa halimashauri ili ziweze kujiendesha.

Amesema yapo mambo mengi ambayo yanapaswa kusimamiwa ipasavyo na viongozi katika ngazi za halimashauri na kudai moja ya eneo ni ujenzi wa mindombinu ambayo imekuwa ikifanywa na wakandarasi ambao wapo wanaokuwa hawafanyi kazi hizo vizuri.

"Zipo sababu ambazo pia zinafanya wakandarasi ambao wanapelekea kushindwa kukamilisha kazi wanaozokuwa wanazifanya ikiwemo kuombwa rushwa za aina mbalimbali pale wanapokuwa wamepewa kazi.

"Nawaomba viongozi wa halimashauri,manispaa na majiji kubadilika na kufanya kazi kwa maadili ya hali ya juu na muwachulie hatua watendaji ambao ni wabadhilifu na waomba rushwa kwenye maeneo yenu,"imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imepewa fursa ya kukusanya kodi za majengo ambazo awali zilikuwa zikikusanywa na halimashauri kutokana na halimashauri nyingi kushndwa kukusanya mapato hayo na kupelekea mapato mengi kupotea.

Akizungumza kwenye mkutano huo,Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania(ALAT)Stephene Mhapa,amesema serikali serikali inapaswa kutoa mapema na kwa wakati ruzuku kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ili iweze kukamilka kwa wakati.








Amesema miradi mingi imekuwa ikikaa kwa muda mrefu bila kukamilika kutokana na kuchelewa huko kwa fedha na kuomba serikali kuu kulifanyia kazi eneo hilo ili kuweza kuepuka lawama mbalimbali ambazo zimekuwa zikielekezwa kwenye halimashauri.

 Maafisa kutoka benki ya NMB ambao ndio wadhamini wakubwa wa mkutano huo
 Meya wa Manispaa ya Musoma akiwakaribisha wageni kwenye mkutano
 Mkurugenzi wa halimashauri ya Tarime,Apoo Castro Tindwa,akifatilia mkutano wa ALAT
 Sehemu ya wajumbe wa mkutano

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI)George Simbachawene akiwasili kufungua mkutanom kwa niaba ya Rais
 Waziri akisaini banda la Baraza la Famasia



 Burudani ilihusika kwenye mkutano

 Wageni waalikwa pia walikuwepo,(kushoto ni Meya wa zamani wa Manispaa ya Musoma,Alex Kisurura na kulia ni Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mara,Holle Makungu
 Waziri akifungua mkutano
 Sehemu ya wafadhiri wakuu wa mkutano

 Waziri akizindua kitabu kinachozungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya ya Seikali za Mitaa

 Picha za pamoja wajumbe na wadau mbalimbali wakiwa na Waziri na viongozi mbalimbali
 Picha ya pamoja na wadhamini wakuu wa mkutano
 Baadae Waziri alimalizia kwa kuzungumza na Waandishi wa Habari

Post a Comment