0





MBUNGE wa Jimbo la Bunda mjini,Ester Bulaya,kesho ataanza kutoa utetezi wake katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2015 Jimbo la Bunda mjini iliyofunguliwa na wapiga kura 4 inayosikilizwa na Jaji Noel Chocha,wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza inayokaa mjini Musoma.

Utetezi wa Bulaya ambaye ni mlalamikiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo, utaanza mara baada ya jana shahidi wa tatu wa upande wa walalamikaji,Stephine Wasira,kufunga ushahidi wa wapeleka maombi kwa saa 2 ambapo pamoja na mambo mengine alidai palikuwepo na kampeni za wazi wakati wa upigaji kura uliofanywa na badhi ya wasimamizi wa uchagui huo.


Awali mbele ya Mahakama hiyo hii leo,Wakili anayemtetea Ester Bulaya,Tundu Lissu,aliiomba Mahakama kutupilia mbali kesi hiyo kwa kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa waleta maombi hautoshi kuthibisha tuhuma zilizopo kwenye hati ya maombi kwa kiwango kinachostahili.

Alisema Mahakama ipokee hoja kuwa hakuna kesi ya kujibu na maombi yaliyoletwa yafutiliwe mbali bila ya wajibu kujitetea katika kesi hiyo na kudai kuendelea kuwepo ni kupoteza muda.

Post a Comment