0
 KIONGOZI wa mbio za mwenge,Amour Hamad Amour,amekipongeza kiwanda cha mafuta ya alzeti cha Sunlishe kilichopo Nyamongo wilayani Tarime kwa kufanya uwekezaji mzuri na kuendana na mpango wa serikali ya awamu ya tano inayosisitiza ujenzi wa viwanda na kuuomba uongozi wa kiwanda hicho kupanua wigo zaidi wa uzalishaji ili waweze kuwahudumia wananchi wengi zaidi.

Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho,Josephat Muniko,amesema moja ya malengo ya mradi  ya kiwanda ni kukamua mafuta yenye ubora yenye kukidhi hadhi ya kimataifa na kutengeneza ajira kwa jamii inayozunguka mradi na kuhamasisha jamii kulima zao la alizeti ambalo soko lake ni la uhakika
 Viongozi wakitembelea kiwanda hicho
 Kiongozi wa mbio za mwenge katika picha ya pamoja na uongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha Sunlishe
 Kazi inaendelea
 Kiongozi wa mbio za mwenge akipewa zawadi ya box la mafuta kutoka uongozi wa kiwanda
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime,Glorious Luoga,akikabidhiwa zawadi yake
 Apoo Castro Tindwa,mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime nae alipata zawadi
 Baada ya kutoka kiwandani burudani ziliamia uwanja wa mkesha wa mwenge Nyamongo ambapo kiongozi wa mbio za mwenge aliongoza upande wa burudani


Post a Comment