0





 JUMLA ya matukio 116 ya ukatili wa kijinsia yamelipotiwa wilayani
Rorya huku wengi waliofanyiwa ukatili huo wakiwa ni wanawake hali
iliyopelekea masister wa Moyo Safi wa Maria Afrika wa Musoma kufanya
kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia kwenye wilaya hiyo.

Akizungumza kwenye semina ya viongozi wa serikali ya vijiji
iliyofanyika Kijiji cha Irienyi Kata ya Nyamaguku wilaya ya Rorya,
kiongozi wa masister hao, Janepha Mabonyesho, amesema pamoja na elimu
Mungu wanayotoa lakini pia jamii inapewa elimu kuhusiana na kuachana
na kutendeana matukio ya kikatili.


Amesema viongozi wa vijiji ni moja ya njia rahisi ya kufikisha ujumbe
kwa jamii kwa kuwa wanakaa nao kwenye vikao mbalimali mara kwa mara na
kudai semina hiyo itawasaidia kuwajengea uwezo wa kuendelea kutoa
elimu hiyo.


Amesema wapo viongozi ambao wanaona na kuyashuhudiwa matukio ya
ukatili yanayotokea kwenye jamaii na kuyafumbia macho kutokana na
wengine kuwaogopa waaotenda matukio hayo hivyo semina ya kuwajengea
uwezo itasaidia kuyatolea taarifa na wahusika kuchukuliwa hatua za
kisheria.

Mabonyesho amesema matukio 116 ya ukatili kwa kipindi cha miezi 3 ni
mengi na kudai jitihada za pamoja zinapaswa kuchukuliwa ili kuweza
kuzuia matukio hayo kwa kuwa yanapelea kudumaza nguvu kazi ya taifa na
kuifanya jamii kuishi kwa mashaka.


“Tunalishukuru shirika la The Foundation Civil Society kwa kutuwezesha
kwenye kampeni hii na kwa kuwashirikisha viongozi hawa wa vijiji ambao
kwa asilimia kubwa wanaishi na jamii tutaweza kufanikiwa kumaliza
vitendo vya ukatili vinavyotokea kwenye wilaya hii.



“Baada ya viongozi hawa wa vijiji tutakaa pia na wazee wa mila na
makundi mbalimbali ili kuwapa elimu juu ya athari za kutendeana
matukio ya ukatili na tukishirikiana kwa pamoja ni imani yetu
tutayamaliza matukio haya.”alisema Mabonyesho.

Mratibu wa kampeni hiyo, Nollasko Mgimba, amesema katika awamu ya
kwanza kampeni hiyo inaendeshwa kwenye kata 7 na vijiji 25 kati ya
Kata 13 ambapo elimu imekuwa ikitolewa na jamii imeonekana kuipokea
kwa kujitokeza kwa wingi katika semina za utoaji elimu.


Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Rorya ambaye pia
ni mratibu wa dawati la jinsia la halmashauri hiyo, Mwema Salum,
amesema katika kuhakikisha matukio hayo yanayokomeshwa wameanzisha pia
club za kupinga ukatili kuanzia mashuleni ili kuweza kutoa elimu hiyo
zaidi.


 









Post a Comment