0
 ABIRIA wanaofanya safari katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Musoma, leo wamepata usumbufu mkubwa baada ya gari zinazofanya safari kwenye maeneo mbalimbali kugoma kwa kile walichokida kupunguziwa nauli na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na hivyo kuwapa hasara kwa huduma wanazozitoa.

 Madai ya kupunguzwa kwa nauli yamepingwa vikali na Meneja wa Sumatra mkoa wa Mara, Halima Lutavi na kudai nauli zilizopo zipo kwa mujibu wa sheria na wao wamekuwa wakizisimamia ili abiria wasiweze kuumizwa na nauli kubwa
 Meneja wa Sumatra amesema watakutana na wamiliki wa magari ili kuweza kulizungumzia suala hilo ili wananchi waendelee kupewa huduma kama kawaida
 Bei zinazotambuliwa na Sumatra ambazo wamiliki wa magari wamekuwa wakizipinga

Meneja wa Sumatra mkoa wa Mara, Halima Lutavi, ambaye amesema amambo mengine wanayoyasimamia ni kuhakikisha abiria wanalipa nauli halali na kupewa tiketi zenye majina ya abiria pamoja na usafi wa madereva na kondakta ambalo wamekuwa wakisimamia

Post a Comment