KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imeunga mkono juhudi za serikali katika uandikishaji wa watoto wenye umri chni ya miaka 5 ili wapate vyeti vya kuzaliwa kwa kutoa simu za mkononi 1175 zenye thamani ya shilingi milioni 77 ili kuwawezesha ma afisa usajili kutuma taarifa za usajili kila unapofanyika. |
Mmoja wa wasanii kutoka mkoani Simiyu akionyesha umahili wa kucheza na nyoka katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo mjini Musoma
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk.Vicent Naano akizungumza na kuwakaribisha wageni mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi huo
Meya wa Manispaa ya Musoma, Kapten mstaafu, Patrick Gumbo, akitoa shukrani kwa wageni mbalimbali waliofika Musoma kwaajili ya zoezi la uzinduzi wa usajili na uandikishaji wa watoto walio na umri chini ya miaka 5 ili waweze kupata vyeti vya kuzaliwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju, akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo amedai vyeti hivyo vina umuhimu mkubwa na kuwahimiza wazazi na walezi kujitokeza kuwaandikisha watoto
Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Joseph Mutalemwa (katikati) akifatilia uzinduzi huo
Ufatiliaji
Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akiashiria uzinduzi wa zoezi hilo ambapo amesema zoezi hilo ni muhimu kwa serikali katika kufanikisha mipango mbalimbali kwa kuwa itakuwa inawajua watu wake kutokana na zoezi hilo pamoja na mengine yanayofanywa na serikali na kuwahimiza wananchi kujitokeza kuwasajili watoto na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa kuwa ni haki yao ya msingi
Post a Comment
0 comments