SHINDANO la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Mara " Miss Mara 2018" limezinduliwa rasmi na mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, ili kutoa furasa ya kufanyika michakato mbalimbali hadi kufikia siku ya shindano lililopangwa kufanyika tarehe 7/7/2018 katika Manispaa ya Musoma huku waandaaji wa shindano hilo kampuni ya Spece 2000 Co Ltd yenye uzoefu wa masuala ya burudani wakiahidi kurejesha hadhi ya shindano hilo kama ambayo walivyoaminiwa na kampuni ya Look chini ya Basira Mwanukuzi ambao ndio waandaaji wapya wa Miss Tanzania. |
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa shindano hilo uliofanyika kwenye hotel ya Le Grand mjini Musoma,mkuu wa wilaya hiyo, Dk.Vicent Naano, amesema kapuni hiyo itafanikiwa kurudisha hadhi ya mashindano hayo ikiwa itafanikiwa kumpata mrembo anayekidhi vigezo na atakayepatikana kwa haki bila kufanya shindano la ubabaishaji na kumpanga mshindi. Amesema yupo tayari kuwaunga mkono waandaji wa shindano hilo na kuwaunganisha a wadau mbalimbali kwa kuwa hana wasiwasi na waandaaji katika masuala ya burudani na kuwataka kuzunguka mkoa wote wa Mara kwenye wilaya zake kusaka washiriki wa shindano hilo. |
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Spece 2000 Co Ltd, Abubakar Nyamakato, amesema kutokana na kuaminiwa na kampuni ya Look katika kuandaa shindano hilo mwaka huu,wamekusudia kufanya shindano la mfano na watazingatia vigezo vyote ambavyo vinahitaji
Amesema moja ya malengo ambayo mshindi wa miss Mara atakayepatikana ni kuhakikisha anakuwa barozi mzuri wa kuuwakilisha mkoa wa Mara hususani katika masuala ya utalii wa ndani kutokana na rasilimali zilizopo na kupingana na masuala ya ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo
Meneja wa kampuni ya Spece-Big Hassan akiwa ametulia kwenye uzinduzi huo |
MC Kiokote akiendesha uzinduzi huo huku juu wadau mbalimbali wakifatilia uzinduzi huo
Mkurugenzi Abuu akizungumza kwenye uzinduzi huo |
Mkuu wa kitengo cha matangazo miss Mara 2018, Shomari Binda akitoa maelezo kuhusiana na shindano hilo.
Mkuu wa wilaya akizungumza kwenye uzinduzi huo |
Wadada wa kampuni ya Spece wakipata vitafunnwa
Mkuu wa wilaya akiwa na wakurugenzi wa kampuni ya Spece ambao ndio waandaaji |
Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi huo |
Wafanyakazi wa kampuni ya Spece wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi |
Mambo ya sausage zilihusika kutoka Le Grand Hotel |
Ma selfeeee yalihusika |
Mambo ya kubadilishana mawazo |
Post a Comment
0 comments