0


KAMATI za kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya wilaya ya Rorya zimepewa mafunzo ya kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia ili ziweze kufanya kazi na kutolea taarifa vitendo vyote vya ukatili.
Mafunzo hayo yametolewa kwenye kamati hizo ukiwa ni mwendelezo wa elimu kwenye makundi mbalimbali yanayotolewa na shirika la Masister wa Moyo Safi wa Maria (Baraki Sisters Farm) kwa ufadhili wa shirika la The Foundation For Civil Society.
Akizungumza wakati wa utoaji wa mafunzo hayo, Mratibu wa mafunzo hayo, ,Nollasco Mgimba, amesema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa kamati za ulinzi wa wanawake na watoto na zitawasaidia katika utoaji wa taarifa.

Amesema ukatili unaanzia kwenye familia na mafunzo hayo yamelenga namna ya utoaji wa taarifa na yamewashirikisha jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia ambao wamesaidia kutoa muongozo namna ya utoaji wa taarifa pale wanapoona matukio ya ukatili.
Wakizungumza mara baada ya kupokea mafunzo hayo, wanakamati hao kutoka vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika utoaji wa taarifa maana kabla ya kupokea mafunzo hayo walikuwa hawana uelewa wowote.

Post a Comment