NA SHOMARI BINDA-MUSOMA
BENKI ya
CRDB tawi la Musoma imeanza kutoa mikopo ya pikipiki ya magurudumu
matatu(bajaj) pamoja na zile za magurudumu mawili kwa wajasiliamali vijana
lengo likiwa ni kuwawezesha kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Utaratibu wa
benki hiyo umeanza kwa kuwawezesha wajasiliamali watatu kwa kuwakabidhi
pikipiki 3 zenye thamani ya shilingi milioni 21 na kudai mikopo hiyo ni
endelevu kwa wateja wake ambayo italipwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo, meneja wa benki ya CRDB tawi la
MusomaWilfred Massawe, alisema wanaunga mkono juhudi za serikali katika
kuwaondolea umasikini watanzania na mikopo hiyo waliyoitoa ikitumiwa vizuri
itainua kipato cha familia.
Alisema
kabla ya wahusika kukabidhiwa mikopo hiyo ya pikipiki za miguu mitatu wahusika
walipewa elimu ya matumizi mazuri na namna ya kufanya biashara hiyo ya
usafirishaji na iwapo watazingatia mradi huo utawatoa sehemu moja kwenda
nyingine.
Massawe
alisema mikopo hiyo ina tija na lengo lake ni kuinua uchumi wa wateja wake na
wananchi huku marejesho yake yakiwa ya muda mrefu na kusisitiza matunzo mazuri
ya pikipiki hizo ili malengo yake yaweze kutimia.
“
Tumekabidhi pikipiki hizi za magurudumu matatu kwa wateja wetu kama mkopo
kwaajili ya kuongeza kipato chao na mikopo hii ni endelevu tukiunga mkono
juhudi za serikali katika kuinua kipato cha wananchi”,alisema Massawe.
Meneja wa
biashara wa benki hiyo tawi la Musoma, Muzi Naugali, alisema biashara hiyo ya
usafirishaji iwapo itatumiwa vizuri na wahusika itawanufaisha na hata kuongeza
biashara nyingine kutokana na pikipiki hizo.
Kwa upande
wake meneja mikopo wa benki hiyo, Alexander Reuben, alisema elimu juu ya
matumizi bora ya mikopo wameitoa na kuwa na imani wahusika wataitumia kufanya
marejesho na kuyakamilisha hatimaye kuzimiliki pikipiki hizo.
Post a Comment
0 comments