news SHOMMI B 0 6:32 AM Serikali imewasimamisha kazi Maafisa wa Ngazi za juu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika hatua muhimu ya kumaliza mgomo wa madaktari unaoendelea hapa nchini . Akitangaza uamuzi wa serikali Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyewatembelea madaktari waliogoma, amewataja waliosimamishwa kazi mara moja kuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Dk Deo Mtasiwa. Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wanasimamishwa kazi ili pia kupisha uchunguzi dhidi yao kwa vile pia wana tuhuma nyingine kinyume na maadili ya kazi. Waziri Mkuu Pinda amesema wengine wanaotarajiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kusubiri uamuzi wa Rais, ni pamoja na Waziri wa Afya Dk Haji Mponda na Naibu wake Dk Lucy Nkya. Mgomo wa madaktari ambao umedumu nchini Tanzania kwa takriban wiki tatu sasa umesababisha kuzorota kwa huduma mbalimbali katika hosptali za umma na nyingine kufunga vitengo muhimu. Madaktari hao wanadai nyongeza ya mishahara, mazingira mazuri ya kazi pamoja na marupurupu mengine ambapo serikali imekubali kuyashughulikia. Katika makubaliano na Waziri Mkuu madakatari waliogoma wamekubali kumaliza mgomo na Ijumaa hii wanatarajiwa kurejea kazini. news Serikali imewasimamisha kazi Maafisa wa Ngazi za juu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika hatua muhimu ya kumaliza mgomo wa mad... Soma Zaidi...>>.
NEWS SHOMMI B 0 2:28 AM MTOTO ANASULIKA KIFO BAADA YA KUTUPWA CHOONI. Na-Shomari Binda Musoma. Mtoto wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu amenusulika kifo baada ya kutopwa katika shimo la choo na kuokolewa na wasamalia wema. Tukio la kutupwa kwa mtoto huyo lilibainika leo asubuhi katika mtaa wa bandarini kata ya iringo katika manispaa ya Musoma. Akizungumza na blog hii mmoja wa shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la mama Torry alisema kuwa alisikia kilio cha mtoto kikitokea katika shimo la choo alipokuwa akifanya usafi majira ya saa 12 asubuhi na ndipo alipoamua kuwajulisha majirani kwa ajili ya msaada zaidi. Shuhuda huyo aliongeza kuwa baada ya majirani kufika walifanya jitihada za kubomoa mfuniko wa shimo la choo hicho na kufanikiwa kumtoa mtomto huyo akiwa mzima. Kwa upande wake Hamisi Bobera ambye pia alishuhudia tukio hilo alisema kuwa nusura ya mtoto huyo ilipatikana baada ya choo hicho kuanza kutumika hivi karibuni licha ya kuwa na kina kirefu. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Mara kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Robert Boaz alisema kuwa wananchi watakaokuwa wanatambua mama au mlezi ambaye alikikuwa na mtotot na kwa sasa hayupo nae kutoa taarifa polisi au serikali za mtaa ili waweze kumbaini aliyehusika na tukio hilo. Kamanda boazi alisema mtoto huyo kwa sasa amekabidhiwa katika timu ya ulinzi wa mtoto ya manispaa ili aweze kutafutiwa hifadhi huku jitihada za kumtafuta aliyefanya kitendo hicho zikiendelea. Wakati huo huo kamanda wa polisi mkoani Mara alisema kuwa mtu mmoja mwanaume ameokotwa akiwa amekufa na kuaribika katika kijiji cha kenyamota wilayani Serengeti na kushindwa kutambulika. Alisema kuwa mtu huyo alikuwa amevaa suruali ya langi ya udongo na shati nyeupe yenye ufito mwekundu kifuani na kuwataka wananchi ambaye wanaweza kuhusiana na mtu huyo kuwasiliana na jeshi la polisi ili kufanya uchunguzi zaidi wa kifo cha mtu huyo. NEWS MTOTO ANASULIKA KIFO BAADA YA KUTUPWA CHOONI. Na-Shomari Binda Musoma. Mtoto wa kike anayekadiliwa kuwa na umr... Soma Zaidi...>>.
news SHOMMI B 0 6:36 AM CHAKULA CHA MSAADA CHAZUA GUMZO BARAZA LA MADIWANI Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini Dk. Kalaine Kunei amesema kuwa suala la ucheleweshwaji wa Mahindi ya chakula cha msaada ni la Kitaifa na si mzabuni aliepewa tenda ya kusambaza mahindi hayo. Hayo ameyasema leo katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbu wa mikutano wa Halmashauri hiyo. Amesema kumekuwa na upungufu katika ghala la Taifa la chakula Mkoani Shinyanga kutokana na kuhudumia mikoa ya Kanda ya Ziwa hali ilipelekea kuwepo na foleni ya Magari Mkoani humo inayosubiri kupatikia mahindi hayo. Dr. Kunei amesema kuwa baadhi ya Kata katika Halmashauri hiyo ya Musoma zimekwisha pata Mahindi hayo na zile ambazo bado hazijapata zinaendelea kushughulikiwa. Awali Diwani wa Kata ya Nyamimange Nyaswe Chacha alihoji kitendo cha baadhi ya Kata kupewa mgawo wa mahindi mara mbili wakati Kata nyingine zikiwa bado hazijapata hali iliyopelekea baadhi ya madiwani wengine kulizungumzia suala hilo. Akizungumzia suala la Elimu Katibu tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma Bi. Debora Makinga ameomba madiwani wa Halmashauri hiyo kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyobaki ili kila mwanafunzi aliefaulu kwenda Sekondari aweze kupata nafasi hiyo. news CHAKULA CHA MSAADA CHAZUA GUMZO BARAZA LA MADIWANI Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini Dk. Kalaine... Soma Zaidi...>>.
SPORTS SHOMMI B 0 12:28 AM POLISI MARA BINGWA LIGI YA WILAYA Timu ya maafande wa polisi Mara wametangazwa kuwa mabingwa wa ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Musoma baada kumaliza ligi hiyo kwa kufikisha pointi 30 kutoka na michezo 10 waliyoshuka dimbani. Polisi Mara ambayo kwa mwaka huu imepania kufika mbali imeanza kuonyesha dhamila yao katika ligi ya wilaya iliyomalizika katika uwanja wa kumbukumbu ya karume mjini hapa baada ya kuzifunga timu zote zilizoshiriki katika ligi hiyo. Akitoa vyeti vya ushiriki kwa timu zilizoshiriki ligi hiyo mwenyekiti wa chama cha soka manispaa ya Musoma(FAMT)Dedid Sungura alizitaka timu zote zilizopata kushiriki ligi ya taifa ngazi ya mkoa wa Mara itakayoanza hivi karibuni kujipanga na kufanya maandalizi mazuri ili ziweze kufanya vuzuri katika ligi hiyo. Sungura amwezitaka timu za polisi,kigera fc na Musoma shoting kufanya usajili makini na kuwashirikisha wanachama wao na wadau wengine ili kuwaongezea nguvu ya kufanya maandalizi kabla ya kuanza kwa ligi ya mkoa. Kwa upande wake msemaji wa timu ya polisi Mara Musa Masoud(keita)akizungumza na Tanzania daima alisema kuwa baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya Taifa ngazi ya wilaya sasa nguvu zao wamezielekeza katika ligi ya mkoa ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki ligi ya Taifa ngazi ya Taifa. Keita alisema kuwa wamedhamilia kwa msimu huu kufanya vizuri katika hatua mbalimbali baada ya kupata ushirikiano kutoka kwa kamanda wa polisi mkoani Mara Robart Boaz na wadau wengine wa timu hiyo na kuwataka wachezaji wengine wanaotaka kujiunga na timu hiyo wafike katika mazoezi yatakayoanza hivi karibuni baada ya mapumziko ya kumalizika kwa ligi ya wilaya. SPORTS POLISI MARA BINGWA LIGI YA WILAYA Timu ya maafande wa polisi Mara wametangazwa kuwa mabingwa wa ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya... Soma Zaidi...>>.
home SHOMMI B 0 2:34 AM WANASHERIA WASIKITISHWA NA ASKARI POLISI KUWA MAHAKIMU Na-Shomari Binda Musoma CHAMA cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Mkoa wa Mara wameonesha kusikitishwa na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani wanaosimamia na kuhakikisha matumizi bora na sahihi ya barabara wamegeuka kuwa hakimu wa makosa yote, pia wamepinga adhabu kwa mtu aliyehukumiwa kuua kwa kukusudia ahukumiwe kifo na kusema kuwa hiyo sio sahihi na wala haki. Kauli hiyo ilitolewa na Wakili Baraka Makoye kwa niaba ya chama hicho ambapo alisema kuwa askari hao wa barabarani wamekuwa wakitoza faini kwa kwa mamlaka ambayo wamepewa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ambaye ni OCD na siyo Kamanda wa usalama barabarani (OCS), kamanda wa usalama barabarani Mkoa (RTO) au mwingine yeyote. “Baya zaidi kanuni za utoaji adhabu hazifuatwi wakati sheria inaelekeza vipi atendewe mkosaji wa mara ya kwanza, mkosaji mzoefu na kuwa kiwango gani cha adhabu kitolewe wenzetu leo kila kosa utoza faini ya shilingi 30,000,”alisema Wakili Makowe. Alisema kuwa maudhui ya siku ya sheria nchini yanayohusu faida za adhabu mbadala kwa jamii, hazitakosewa wakiendelea kusisitiza kuwa adhabu huambatana na hatia na shurti itamkwe na kutolewa na na taasisi yenye mamlaka hayo kisheria. “Si kwa sera, mazoea au matakwa, kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume cha sheria, natenda kwanza tujikite katika utoaji wa adhabu mbadala ndipo tuangalie faida husika. Kwa kuwa jambo hili ni pana, juhudi za kulichambua kwa undani zitafanyika liingiliane na mambo mengine na hivyo huenda ikaathiri mtiririko wa uwasilishaji wa mada lakini nina imani tutagusa sehemu zote muhimu,”alisema. Alisema kuwa kutokana na kupitia maudhui ya Adhabu mbadala katika kesi za jinai, na faida zake kwa jamii kwa niaba ya chama cha mawakili wa Tanganyika muda muafaka umefika na vifungu vya 197 na 26 (1) vya sura ya 16 ya sheria za nchi vitazamwe upya. “Ni muda muafaka kwa adhabu mbadala itumike na iamriwe hadi kugusa kesi za mauaji ya kukusudia, pia kwamba hata vile vifungu vya 195 (1) na 198 vya sheria hiyo navyo vitazamwe upya. Kwamba si jambo jema mtu akae gerezani hadi atakapokufa adhabu mbadala yaweza kutolewa kwake,” alisema. Naye Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mkoa huo, Hussein Mushi alisema kuwa adhabu mbadala inafaida nyingi katika jamii ambapo baadhi ya faida ni pamoja na kupunguza msongamano magerezani, kulipunguzia serikali gharama za kuendesha magereza kwa kupunguza watu wanaotegemea huduma magerezani. “Hii ni pamoja na kuishirikisha jamii kwa kuwarekebisha wahalifu na kuwawezesha wahalifu kuendelea kutunza na familia zao huku wakiendelea kutumikia vifungo vyao, kutoa mchango wa maendeleo kwa jamii pale wafungwa wa kifungo cha nje wanaposhiriki katika ujenzi wa wa shule, hospitali, barabara, utunzaji wa mazingira na usafi katika ofisi za umma hali itakayoipunguzia serikali gharama za shughuli hizo, alisema Mushi. Pia alitoa onyo kwa wananchi kuacha tabia ya kuingilia shughuli za huduma za jamii wajue kuwa ni kinyume cha sheria na ni kosa la jinai na mtu anapotiwa hatiani atapaswa kulipa faini ya shilingi Laki 5 au kifungo cha miaka miwili jela au vyote viwili. leo ilikuwa ni siku ya sheria nchini na kuashiria mwanzo wa shughuli za mahakama kwa mwaka 2012 ambapo maudhui yake ni adhabu mbadala katika kesi za jinai, Faida zake katika jamii ambapo hufanyika mwezi wa pili wa kila mwaka MWISHO home WANASHERIA WASIKITISHWA NA ASKARI POLISI KUWA MAHAKIMU Na-Shomari Binda Musoma CHAMA cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Mkoa wa Mara w... Soma Zaidi...>>.