Amuuwa mtoto kwa kumchapa fimbo
Mwingine auwawa kwa kuchomwa moto akituhumiwa ujambazi
Na Shomari Binda,Musoma
MKAZI
mmoja wa kata ya Nyasho katika Manispaa ya Musoma aliyefahamika kwa
jina la Yohana Msafiri (38) amemuuwa mtoto wake Veronica Yohana kwa
kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake Desemba 23 na
kupelekea kifo chake akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuzidiwa
na maumivu.
Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari,Kamanda wa
Jeshi la Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma alisema tukio hilo
lilitokea majira ya saa 5 usiku
katika maeneo hayo ya Nyakato ambapo chanzo cha kuchapwa viboko kwa
mtoto huyo na matatizo ya kifamilia.
Alisema mzaza wa Mtoto huyo
anashikiliwa na Jeshi la
Polisi kutokana na tukio hilo ambapo amedai mara baada ya kukamilika
kwa upelelezi mzazi huyo atafikishwa Mahakamani kuweza kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Kutokana na tukio hilo Kamanda Mwakyoma amewataka
wazazi kuangalia adhabu mbadala ambazo wanaweza kuwapa watoto pale
wanapokuwa wanafanya makosa katika kuwafunza na sio kuwa na hasira
ambayo inaweza kupelekea madhara mengine makubwa zaidi.
"Wazazi
lazima waangalie adhabu mbadala ambazo zinapaswa kupewa watoto pale
wanapofanya makosa maana kwanza ifahamike hawa ni watoto na yaale
wanayoyafanya ni kutopkana na utoto wao hivyo iwepo busara katika kutaka
kutoa adhabu kwa watoto wetu,"alisema Kamanda Mwakyoma.
Katika
tukio lingine Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara alisema mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Gogogo anayekadiliwa kuwa na umri kati
ya m,ika 40 na 45 mkazi wa Bunda aliyekuwa akiishi kata ya Nyakato
Mshikamano katika Manispaa ya Musoma aliuwawa kwa kushambuliwa na
kuchomwa moto kwa kudaiwa anahusika katika matukio ya ujambazi.
Kamanda
Mwakyoma alisema Wananchi wanapomuhisi mtu anashiliki katika matukio ya
uhalifu ni vyema kutoa taarifa Polisi na si kujichukulia sheria mkononi
kwani hata kama mtuhumiwa anashiliki anapokamatwa anaweza kutoa taarifa
ambazo zinaweza kuwapata watu wengine ambao anashiliki nao katika
matukio hayo.
Alisema kujichukulia sheria mkononi ni kosa kwa
mujibu wa sheria na atakaye kamatwa kutokana na kosa la kujichulia
sheria mkononi atafikishwa Mahakamani kutokana na kosa hilo na kutoa
tahadhari kwa Wananchi kuacha tabia hiyo kwani haifai na sheria
hairuhusu kujichukulia sheria mkononi.
Post a Comment
0 comments