Profesa Muhongo aijibu CUF kuhusu mgawo wa umeme
Na Shomari Binda,
Musoma
WAZIRI
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kuwa hakuna
hoja ya mgawo wa umeme kwa sasa hapa Nchini kutokana na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) kujipanga kutafuta vyanzo vingine vya uzalisha
mbadala wa umeme kuliko kutegemea maji ili ifikapo Mwaka 2013 Tanzania
iweze kupata umeme wa uhakika.
Kauli hiyo ameitoa Mjini hapa
katika kikao kilichowashilikisha Vijana wa Manispaa ya Musoma kutaka
kujua ni changamoto
gani zinazopelekea Mji huo kukosa Maendeleo na kuzungummzia jinsi
Shirika hilo linavyoendeleaa kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali
ya kiutendaji ili
kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kupata umeme wa uhakika.
Alisema
anapingana na maazimio yaliyotolewa na Chama cha Wananchi (CUF) katika
Baraza lake Uongozi lilofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam na
kueleza kuwa upo mgawo usio rasmi wa umeme ambao unapelekea kero kwa
Wananchi na kukwamisha shughuli za kimaendeleo ambazo zinahitaji nishati
ya umeme.
Profesa Muhongo alisema suala la kukatika kwa umeme
kwa dakika mbili ama tatu sio mgawo kama inavyoelezwa na Chama hicho
bali ni kutokana na miundombinu ambayo imechakaa ambapo kwa sasa Tanesco
imeelekeza katika kufanya jitihada za kuibadilisha ili kuweza
kukabiliana na changamoto hiyo.
''Sote tunafahamu miundombinu ya
Shirika hili mingi imechakaa na inahitaji mabadiliko ambayo kwa sasa
kwa asilimia kubwa inafanyiwa kazi hivyo inapelekea kuwepo na kero ya
kukatika kwa umeme kwa muda furani lakini sio kila siku na huo sio mgawo
wa umeme jamani tuache propaganda za kisiasa katika
masuala mengine ya maslahi ya Taifa,"alisema Muhongo.
Alisema
yeye akiwa kama Waziri mwenye dhamana ya umeme atamueleza Waziri Mkuu
ama Rais iwapo kutakuwa na mgawo wa umeme lakini sio watu kusimama na
kusema kuna mgawo kitu ambacho amekiita ni uzushi ambao unatumiwa na
wanasiasa katika propoganda zao ambazo hazina tija kwa Taifa.
Alidai
Tanesco inajipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana na tayari
imeanza programu ya kusambaza umeme Nchi nzima katika Vijiji na Wilaya
na kusema kazi hiyo inahitaji kupana ushirikiano katika kuifanukisha na
kuomba kupata maoni kwa kila Mwananchi namna ambavyo anataka shirika
hilo lifanye katika kuleta ufanisi tofauti na kipindi cha nyuma
Aidha
Profesa Muhongo alisema zipo changamoto nyingine ambazo zinafanywa na
watu wasio wazalendo kwa kuiba mafuta ya Transifoma pamoja na waya za
umeme hali inayopelekea kujitokeza kwa matatizo ya kukatika kwa umeme
ili kupisha mafundi kuweza kurekebisha na
kurudisha umeme na kuwaomba Wananchi kuweza kutoa taarifa pale
wanapoona mtu anataka kuhujumu shirika hilo.
Akizungumzia masuala
ya kimaendeleo katika Mji wa Musoma,Waziri Muhongo aliwataka vijana wa
Mji huo kuacha ubinafsi na kushirikiana katika kujitafutia Maendeleo na
kubadilisha muonekano wa Mji huo na kusisitiza kujiepusha na kukalia
siasa muda wote bali wajishughulishe na shughuli mbalimbali za kujiletea
maendeleo.
Post a Comment
0 comments