0
Na Shomari Binda,Serengeti

ASKARI wawili wa jeshi la polisi katika kutoka mkoa wa Kagera,wamekamatwa wakiwa na meno ya Tembo katika hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Mkurugenzi mkuu wa Tanapa Allan Kijazi,akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema askari hao walikamatwa juzu jioni na akari wa hifadhi ya Serengeti kwa kushirikiana na polisi wa kituo cha Mugumu.

Alisema askari hao walifanikiwa kuwakamata askari wenzao wakati wakipeleleza kuhusu matukio ya wizi wa nyara za serikali hivyo kuwakuta na vipande vya meno ya tembo ambavyo vikiunganishwa yanafikia meno mazima sita.

Alisema majangiri hayo ambao ni askari polisi walikuwa wakisafirisha meno ya tembo kutoka kijiji cha Bunchugu wilayani Serengeti kwenda Mugumu mjini kwa kutumia pikipiki mbili.

Hata hivyo Kijazi alisema polisi na askari wa wanyamapori wamekamata mmoja ya watu walikuwa wakiesha pikipiki na mwingine aliyekuwa amebeba mzigo huo huku mwingine akikimbia.

Alisema watuhumiwa hao baada ya kukamatwa waliwapeleka askari kwa matajiri walikuwa wakipelekewa mzigo katika hotel ya Galaxy ambapo pia wamekamatwa pamoja na gari ndogo.

Alisema baada ya kuhojiwa watu hao wamegundulika kuwa wao ni askari polisi mwenye cheo cha Koplo na Konsitebo kutoka Biharamulo mkoani Kagera.
Alisema baada ya kufanywa kwa mawasiliano na mkuu wa polisi katika eneo walikotoka wamekili kuwa ni askari wake huku akishangazwa kukatwa katika eneo la Serengeti mkoani Mara.

Katika simu zao imeonyesha kuwa walikuwa na mawasiliano na watu walioko kwenye mtandao wa mkubwa wa ujangiri wa meno ya tembo.

“Huu mtandao ni mkubwa san asana na wazi sasa imebainika hata Yule faru George aliyepokelewa na Rais Kikwete ndo walihusiku kumuuawa kwaajili ya kuchungua nyara zake…hii ni hatari kwa kwenzetu polisi kushiriki katika kufanya hujuma kwa taifa lao”alisema Kijazi.

Alisema baada ya mahojiano yanayofanyika kituo kikuu cha Mugumu wilayani Serengeti taarifa kamili ya majangiri hao itatolewa.

“Tunaomba ushirikiano na wananchi ili kuhakikisha kuwa tunalinda rasilimali zetu…kwani bila ushirikiano kamwe hatuwezi kufanikiwa”alisema Kijazi.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema,amethibitisha kukamatwa kwa askari hao huku akisema hatua hiyo imetokana na ushirikiano mzuri kati ya askari polisi na watumishi wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti SENAPA ambao umewezeshwa kukamatwa kwa askari.

IGP Mwema akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana kwa njia ya simu alisema kuwa ingawa kitendo hicho kimelifedheesha jeshi la polisi lakini kamwe jeshi hilo halitakata tama kwa kuwaondoa kazini askari wake wanakwenda kinyume na maadili.

“Jeshi la polisi tumekuwa na ushirikiano mzuri na wenzetu wa Tanapa hata kukamatwa kwa askari hawa wawili kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya polisi Mugumu na watumishi wa hifadhi ya Serengeti”alisema IGP Mwema kwa njia ya simu.

Alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na Tanapa limekuwa likiendesha mazoezi mbalimbali ya kupambana na ujangiri katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kamwe haliwezi kurudi nyuma kwa utovu wa nidhamu ambao umeonyeshwa na askari hao.

“Ndani ya jeshi tuna progarammu ya kutoa zawadi kwa kila askari wanaofanya vizuri katika kupambana na uharifu pia kwa wale waokwenda kinyume tumekuwa tukiwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi”alisema Mwema.

“Mpango wa kutii sheria bila shuluti pia unawalenga askari hivyo nakuhakikishia kuwa lazima tutalisafisha jeshi letu la polisi kama kuna askari anajijua hawezi kwenda na kasi hii ya sasa ni vema akajiondoa mwenyewe”alisema IGP Mwema.

Hata havyo ameomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kupambana na vitendi vya uhalifu katika maeneo yao na ujangiri katika hifadhi za taifa.

Kuhusu maua ya kikatili yanayoendelea mkoani Mara,IGP amesema tayari jeshi la polisi limetuma timu maalum ya kuendesha oparesheni maalum ambayo itahakikisha inakomesha unyama huo.

“Tulituma timu ya kwanza ya kukusanya taarifa sasa tumetuma timu kubwa ya kufanya oparesheni kubwa na ya aina yake ili kuhakikishaji kila alihusika anakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria lakini pia ni vyema wananchi wakatoa ushirikiano wakati wa kazi hiyo kubwa na vikundi vya ulinzi pia vifanye kazi yake”alisema mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini.

Mwisho



Post a Comment