Na Shamari
Binda,Tarime
ZAIDI ya malori
30 yenye nafaka ya mahindi yamekatwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tarime
na Rorya kwa madai ya kuingiza nafaka hiyo kutoka nje ya nchi bila kufuata
taratibu.
Umoja wa
Wafanyabiashara,Wakulima na Wadau wa Chakula wa wilaya ya Tarime wamelalamikia
hatua hiyo kwa madai kuwa mahindi hayo yamekuwa yakinunuliwa katika vijiji
ndani ya wilaya ya Tarime ili yauuzwe katika maeneo yenye njaa ndani na nje ya mkoa
wa Mara lakini Polisi na TRA wameyakata kwa madai kuwa yametoka nje ya nchi
Katika barua
yao kwenda Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime,TRA, mamlaka ya chakula na dawa
TFDA na ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime,umoja huo umetaka kupewa ufafanuzi
juu ya kukamatwa kwa nafaka hiyo wakati ikiwa ndani ya nchi.
Katika barua
hiyo iliyosainiwa na katibu wa Umoja huo Chacha Suguta,ambayo BLOG HII imepata nakala yake imetaka kupata ufafanuzi kama kuna zuio lolote
lililotolewa rasmi na Wizara ya Kilimo na Chakula kwaajili ya kuendesha zoezi
hilo la kuzuia kuuzwa maeneo mengine ya nchi yenye njaa chakula hicho.
Aidha
wamesema kuwa hatua hiyo pia inalenga kuwanyima haki wafanyabiahara,wakulima na
wadau wa nafaka jambo ambalo pia litawafanya wapate hasara kubwa.
Kwa mujibu
wa barua hiyo umoja huo umedai kuwa umeambiwa kuwa mahindi hayo yana sumu na
kwamba hayapaswi kuuzwa katika maeneo mengine jambo ambalo wamepinga na kuitaka
Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa kauli
hiyo.
“Sisi tuna
nunua mahindi kutoka katika meneo ya Vijijini kwenye maghala na tunafuata
taratibu zote za usafirishaji ikiwemo kulipia ushuru wa mazao katika maeneo
husika sasa tunashangaa (TRA) kuhusika na kusafirishwa mahindi,mara ya kwanza
tuliambiwa yanatoka Kenye tulipowabana huku tukionyesha vibali na barua toka
katika vijiji tena leo wanazuka na jambo la sumu je TFDA inafanya kazi gani na
ni kwanini wasichunguze kuthibitisha kauli yao”ilisema barua hiyo na kuongeza.
“Kule
mpakani kuna ulinzi mkali na kila mamlaka ipo iweje mahindi yakamatiwe kilometa
70 toka mpakani na kurejeshwa wakidai tumepitisha njia za panya….wakati ule
walizuia tusiuze chakula Kenye leo tunanunua vijijini na kupeleka ndani ya nchi
mikoa ya Mwanza na Shinyanga tena tunakamatwa je Tarime ni kisiwa”walihoji.
“Tunaomba
ufafanuzi wa kimaandishi kwa maana ni jambo geni kwetu la TRA kushikilia magari
yetu na wakitutaka tulipe Dolla 5000 kwa kila gari sawa na Shilingi Milioni
nane na watupe walaka unaopelekea kutozwa faini hiyo,”ilisema sehemu ya barua
hiyo.
Suguta kupitia
barua hiyo wamedai kuwa wameshikiliwa
katika mpaka wa Sirari kwa zaidi ya siku sita sasa huku wengi wao wakiwa
wameishiwa hata pesa ya kula na kuwafanya kuishi maisha ya tabu katika maeneo
hayo na kuomba mamlaka za juu kulipatia ufumbuzi suala hilo.
‘’Ikumbukwe
nyaraka zote zinazostahili na zinazoturuhusu sisi kufanya kazi hii halali ili
kujipatia kipato tunazo lakini pia stakabadhi za ushuru wa Halimashauri tunazo
ikiwa ni pamoja na uthibitisho wa vibali mbalimbali vya watendaji wa Serikali
ya Vijiji sasa iweje tunanyanyaswa na Maafisa wa TRA,”ilisema sehemu ya barua
hiyo.
Hata hivyo akizungumzia
suala hilo Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Joseph Kalinga alisema magari hayo
yamekamatwa kutokana na kuingiza nafaka hiyo bila kufuata sheria.
“Sheria
inataka kila kitu kipite katika lango la mpaka hata kama hakitozwi kodi wala
ushuru lakini wenzetu wanatumia njia za panya kuingiza nafaka toka nje ya nchi”alisema
Kalinga na kuongeza.
“Huwezi
kuingiza chakula kwa njia za panya bila kuangaliwa ubora wake hawa jamaa
wanadanganya tu na barua hizo za watendaji,tumefanya uchunguzi mahindi hayo
yametoka Kenya kwa njia za panya sasa kufanya hivyo ni kuvunja Sheria na
tutawatoza faini kulingana na sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka
2004”alisema.
“Ni kweli
magari hayo yamekamatwa na bado oparesheni inaendelea kwa wale wote wanaoingiza
mizigo kwa njia ya magendo hata kama hakilipiwi kodi lazima sheria zifuatwe na
si vinginevyo”alisisitiza Kalinga.
“Hivyo
vibari vya Vijiji walivyo navyo ni danganya toto laiti kama wangekuwa wamefata
taratibu zinazotakiwa hakuna sababu ambazo zingefanya wakamatwe wamekamatwa kwa
kuwa hawajafata taratibu,”aliongeza.
Hata hivyo
alisema licha ya upana wa mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari maafisa wa forodha
katika mpaka huo wamekuwa wakijitoa muanga kwaajili ya kuhakikisha taifa
linakusanya mapato yake ingawa wamekuwa wakipata vitisho na kufanya kazi katika
mazingira magumu.
Kalinga
aliwaomba wafanyabiashara ambao wanadhani endapo wanapata usumbufu wakati
wakipitisha bidhaa ambazo hazilipiwi kodi wala ushuru katika lango la mpaka huo
kutoa taarifa kwake ama kwa mamlaka nyingine zilizopo ili kuhakikisha kila mtu
anafuata sheria za nchi,zikiwemo zile za afrika mashariki.
Sheria ya
forodha ya afrika mashariki ya mwaka 2004 pamoja na mambo mengine inatoa fursa
kwa mamlaka kutoza faini kulingana thamani ya mzigo na msafirishaji pia kutozwa
faini hadi kufikia dolla 5000 kwa mtu yoyote anabainika kupitisha bidhaa kwa
njia za panya.
Mwisho
Post a Comment
0 comments