0
                                 
Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Thomas Boni Yayi, ametoa wito wa kutuma vikosi kusaidia wanajeshi kupambana na makundi ya wapiganaji nchini Mali.  

Wapiganaji hao ambao wanajumuisha wale wa Tuareg, wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.
''Mzozo wa Mali ulikuwa kitendawili cha kimataifa na NATO inapaswa kusaidia kama ilivyo saidia Afrghanistan,'' alisema Thomas Boni Yayi

''Hata hivyo, harakati dhidi ya wapiganaji hao zinapaswa kuongozwa na kikosi cha Afrika,'' aliongeza kusema bwana Yayi.

Mwezi jana Umoja wa Mataifa uliidhinisha mipango ya kutuma takriban kikosi cha wanajeshi elfu tatu nchini Mali.

 Maafisa wa UN wanasema kuwa hawakutarajia wanajeshi hao kutumwa huko kabla ya mwezi Septemba.

Bwana Yayi, ambaye ni rais wa Benin,alitoa wito wake baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper mjini Ottawa.

Wanachama kadhaa wa NATO ikiwemo, Marekani na Ufaransa, wako tayari,kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afrika watakaoshiriki katika harakati hizi za kumaliza uasi, ingawa hawajajitolea kutuma vikosi.
Bwana Harper alisema kuwa Canada , ambayo ni mwanachama wa , Nato, haijatafakari zaidi kuhusu kujihusisha kijeshi nchini Mali.

Post a Comment