0
Na Shomari Binda
        Musoma,

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt,Hussein Ally Mwinyi (Mb) amemteua Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) Deogratus Ibunga Wegina kuwa Mjumbe wa Bodi ya shauri  ya Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Mara.

Katika barua ya uteuzi huo yenye kumbukumbu CHB 49/213/01/91  ilisema uteuzi huo umeanza tangu Januari 7 2013 na kutumikia nafasi hiyo ya Bodi ya Ushauri hadi Januari 7 2016 kwa kufanya kazi za kiushauri katika kubolesha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na wajumbe wengine.

Katika baarua hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo wa Wegina ambaye amekuwa akiandika Makala katika Magazeti tofauti hapa Nchini umetokana na kushiriki kwa ukaribu katika masuala mbalimbali ya Kijamii kwa kutoa ushauri na michango katika kufanisha shughuli za Kimaendeleo.

Akizungumza na BLOG HII,Wegina alisema amepokea uteuzi huo wa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara na kuahidi kushirikiana na wajumbe wengine walioteuliwa kafanya kazi hiyo ili makusudio ya uteuzi huo yaweze kufanikiwa kama ilivyokusudiwa.

"Nashukuru kwa Waziri Mwinyi kuniona na kuniamini kama naweza kumsaidia kazi hiyo na naamini mungu atanisaidia na kuifanya kwa moyo wangu wote kwa kutoa ushauri ambao utabolesha Hospitali ya Mkoa na huduma nyingine muhimu ambazo zinatolewa ndani ya Hospitali.

"Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla kuna watu wengi na nimeshangaa sana kwa Waziri kuniona mimi ninaamini ni kutokana na utendaji wangu wa kazi,sito muangusha Waziri na ntashughulikia majukumu yangu kadri ya uwezo wangu kwa kuwa ninaguswa na Maendeleo ya Mkoa wa Mara.

"Ninao uzoefu wa kufanya kazi katika bodi mbalimbali ambazo nimekuwa nikiteuliwa kwa vipindi tofauti na huko nimefanya vizuri katika kufankisha naamini hata katika hii bodi mpya niliyoteuliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nitaitumikia vizuri kwa kipindi chote cha miaka mitatu kama barua ya uteuzi inavyoeleza,"alisema Wegina.

Alisema uteuzi wake wa Mwisho ulikuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, alipoteuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Luteni Lepillal Ole Moleiment kudhibiti mapato na matumizi katika Shule ya Msingi Mwisenge na kwa kufanya kazi hiyo watu mbalimbali walichukuliwa hatua kutokana na kwenda kinyume na utaratibu wa kazi.

Wegina ambaye amekuwa Kiongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara kwa kipindi cha Miaka sita aliahidi kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia maadili na kutoa ushauri wenye kujenga lengo likiwa kubolesha huduma mbalimbali zinazotolewa katika Hospitali hiyo.

Post a Comment