Na Shomari Binda
Musoma
JESHI la
polisi Mkoani Mara limewakamata watu kumi na tano akiwemo diwani mmoja wa CCM katika kata
ya Mugango wilaya ya Butiama kuhusiana na mauaji ya kinyama na kikatili ambayo
yameibuka hivi karibuni mkoani Mara hasa katika wilaya za Butiama na Musoma.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Mara kamishna msaidizi mwandamizi SACP Absalom
Mwakyoma,amewambia waandishi wa habari mjini Musoma kuwa watu hao wamekamatwa
katika oparesheni kubwa inayoendeshwa na jeshi la polisi mkoa wa Mara na makao
makuu ya jeshi hilo ikiongozwa mkuu wa oparesheni Saimon Siro.
Amemtaja
diwani ni Bw Wandwi Maguru wa kata ya Mugango ambaye amekamatwa jana akiwa ni
miongoni mwa watu kumi na tano ambao tayari wamekamatwa kuhusiana na matukio ya
kuuawa kwa watu kwa kuchinjwa na wauaji kuondoka na baadhi ya viungo vyao.
Siku mbili
zilizopita mkuu wa jeshi la polisi nchini,IGP Said Mwema,aliiambia Radio One
Streo kuwa jeshi hilo limetuma timu maalum ya askari wake ambao wataongeza
nguvu katika Oparesheni kubwa ya kuwasaka watu wanatuhumiwa kwa mauaji ya
kinyama na kikatili yanayoendelea mkoani Mara.
IGP Mwema amesema Oparesheni hiyo kubwa
inafanyika katika maeneo mbalimbali mkoani Mara hasa katika wilaya yalipotokea
mauaji hayo huku akisema hatua hiyo inafanyika baada kukamilika kwa kazi ya
ukusanyaji wa taarifa muhimu ambayo imefanywa na timu ya watalaam jeshi hilo kutoka makao makuu kwa kushirikiana
uongozi wa polisi mkoani Mara.
Kwa sababu
hiyo IGP Mwema amewaomba wananchi,viongozi wa vijiji,mitaa na watu wenye taarifa
kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano wa kutosha ambao utakao wezesha kukamatwa
kwa watumiwa wote ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,
Post a Comment
0 comments