0
CHRISTINA FABIAN,MWANAMKE ALIYETOLEWA JICHO NA MUME WAKE

LICHA YA JICHO MJAREDI ULIFIKA KATIKA MAENEO MENGINE

HAPA YUPO NA WAZAZI WAKE KATIKA OFISI YA WAANDISHI WA HABARI

NIKO NA MWAANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA THE CITZEN BELDINA NYAKEKE TUKICHUKUA DATA KAMILI


HII NDIYO RB YA KUTAFUTWA KWA MUME ALIYEFANYA TUKIO HILI

HAPO KULIA BABA MZAZI WA CHRISTINA AKIELEZEA KUSIKITISHWA NA TUKIO HILO
Na Shomari Binda
         Musoma,

MATUKIO ya Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake bado yanaendelea kutokea katika Jamii hususani Mkoani Mara huku safari hii Mwanamke mmoja Christina Fabiani mwenye umri wa Miaka (27) akitandikwa na mjaredi na aliyedaiwa kuwa ni mume wake Magige Kisyeri na kupelekea kutolewa jicho moja la upande wa kulia.

Akizungumzia tukio hilo mbele ya Waandishi wa Habari,Mwanamke huyo alisema Januari Mosi aliondoka nyumbani kwake anapoishi katika Kijiji cha Baranga Wilayani Tarime kwa lengo la kwenda kumuogesha mama mkwe wake anayeishi katika kijiji hicho  ambaye ni mgonjwa na aliporudi ndipo alipokutana na adha ya kipigo kutoka kwa mume wake.

Alisema aliporudi nyumbani majira ya jioni ya siku hiyo alimkuta mume wake akiwa amesharudi nyumbani na kumwambia kwanini amechelewa kurudi nyumbani lakini akiwa anamjibu kilichopelekea kuchelewa kurudi kutoka ukweni kwake mara akaanza kumchapa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia mjaredi na baadae mjaredi huo aliokuwa akiutumia kufikia katika jicho lake la kulia.

"Niliondoka nyumbani huku nikimuaga mume wangu kuwa nakwenda kumfanyia usafi mama mkwe wangu amabaye ni mama mzazi wa mume wangu....,nilikutana na kazi nyingi za nyumbani na kuamua nizifanye kwanza ndipo nilejee nyumbani kwangu lakini nilipofika nyumbani mwenzangu hakunielewa na wala hakutaka kunisikiliza.

"Aliniambia kwa nini nimechelewa kurudi nyumbani na kuacha mifugo peke yake ikienda katika miji ya watu huku akiendelea kunichapa sehemu mbalimbali za mwili na hakutaka kunisikiliza licha ya kuendelea kumwambia nimekuta kazi nyingi kwa mama ambazo zimenichelewesha,"alisimulia.

Alisema baada ya kuona amempasua jicho alimuacha na asubuhi yake ya tarehe 2 alimchukua na kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Mara kwa ajili ya matibabu lakini walishindwa kumtibu hadi atakapopeleka PF3 kutoka Polisi ndipo atibiwe.

"Tukiwa njiani kwenda Polisi mume wangu aliniambia niandikishe polisi kuwa tumevamiwa na majambazi nami kuamua kusema hivyo Polisi kutokana na mume wangu kunibana na kunitishia na kupewa PF3.

"Tukiwa tunasubili matibabu pale Hospitalini baba yangu tayari alikuwa amepata taarifa juu ya kupigwa kwangu na kwenda kuandikisha kuwa tumevamiwa ndipo alipompigia simu mume wangu kumtaka akabadilishe maandishi Polisi na baada ya hapo aliniaga kwamba anatoka mara moja na hakurudi hadi leo na baba yangu ndio amenihudumia na kufanyiwa oparesheni ya kutolewa jicho,"alisema Christina.

Mwanamke huyo alisema mume wake amekuwa na mazoea ya kumpiga mara kwa mara ambapo kwa mwezi amekuwa akimpiga mara mbili ama tatu na kinachopelekea kupigwa ni makosa madogo madogo yakiwemo kuchelewa kupika chakula,kufungulia mifogo na kuipeleka malishoni.

Alisema kamwe hawezi kurudi kwa Mwanaume huyo ambaye amezaa naye Watoto watatu na kuviomba vyombo vinavyohusika na utetezi wa Wanawake pamoja na vyombo vya sheria kulifatilia suala hilo na kuweza kuchukua hatua zinazo stahili dhidi ya wale wanao wanyanyasa Wanawake.

Kwa upande wa baba mzazi wa Mwanamke huyo,Fabiani Marengo alisema alipata taarifa kutoka kwa majirani juu ya tukio la kupigwa kwa mtoto wake na kuamua kulifatilia na kushangazwa na taarifa zilizoandikishwa na mume wake kuwa wamevamiwa na majambazi.

"Mimi nimelichukulia tukio hili kama la kinyama na baada ya mume wake kukimbia na kumuacha Hospitali nimemtibia kwa kutumia ghalama zangu na nimelazimika kuchukua (RB) Polisi ya kumtafuta ili sheria ichukue mkondo wake lakini siwezi kuzungumzia masuala ya ndoa.

Akizungumzia tukio hilo,Mkurugenzi wa Shirika la kutetea Haki za Wanawake na Watoto la ABC Foundation Robert Moro alisema Jamii haina budi kubadilika kutokana na kujichukulia uamuzi wa kupiga katika suala ambalo linaweza kuzungumzika.

Muro alisema kama ni mume mwenye busara hakupaswa kumpiga Mke wake kwa kuwa alikwenda kumfanyia usafi mama yake ambaye ni mgonjwa na alitumia utaratibu wa kumuaga kabla ya kuondoka na yeye mwenyewe alimruhusu.

Post a Comment