Na Shomari Binda
Bunda,
Watu saba wamefariki Dunia na wengine zaidi ya 40
kujeruhiwa kufuatia mabasi mawili kugongana uso kwa uso katika Kijiji
cha Nyatwali Wilayani Bunda Mkoani Mara.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari Ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara Kamishina
Msaidizi Absalom Mwakyoma
alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11 jioni ikihusisha mabasi
mawili ya Mwanza Coach lenye namba za usajili T 756 AWT aina ya
scania
marcopolo mali ya Halfan Ahmed wa mwanza likitoka Musoma kuelekea
Mwanza pamoja na basi la Bestline lenye namba T 535 AJR lililokuwa
likitokea Mwanza kuelekea Sirari.
Mwakyoma alisema kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mabasi hayo na madereva kutokuwa
makini ambapo yalifika katika eneo la barabara ambayo inafanyiwa ukarabati na kupita kwa mwendo kasi.
"Madereva
wa mabasi yote mawili walikuwa katika mwendo kasi katika barabara ya
vumbi inayofanyiwa ukarabati na hawakuweza kuonana na kusababisha
kugongana uso kwa uso na kupelekea vifo vya watu saba na zaidi ya 40
kujeruhiwa.
"Watu sita walifariki palepele katika eneo la ajali
na mtu mmoja alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika Hospitali
teule ya Wilaya ya Bunda DDH",alisema kamanda Mwakyoma.
Kamanda
Mwakyoma alisema majeruhi wa ajali hiyo wamelezwa katika Hospitali ya
DDH na kati yao wanne kati 14 ambao walikuwa hawajitambui
wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi
kwani hali zao sio nzuri
kutokana na kuvuja damu nyingi na hivyo hospitali ya wilaya ya bunda
kutokidhi mahitaji ya damu .
Alisema miili ya marehemu
imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya
Wilaya ya Bunda na kuwaomba Wananchi kwenda kuitambua.
"Madereva
wote wawili wamekimbia mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo lakini kila
siku tumeendelea kuwahelimisha madereva juu ya mwendo kasi lakini bado
wapo madereva wasiokuwa makini na tutaendelea kuwachukulia hatua kali
wale wote wana kaidi.
"Lakini abiria nao inabidi wasaidie katika
hili wanapoona madereva wanakwenda mwendo kasi mara wamzue na mara
waonapo askari wa usalama barabarani watoe taarifa,"alisema Mwakyoma.
Baadhi ya abiria walikuwemo
kwenye mabasi hayo walisema kuwa mabasi hayo yalikuwa na mwendo mkali
ambapo walijaribu kupiga kelele kuwaambia madereva kupunguza mwendo
lakini hawakuweza kusikilizwa na muda mfupi ajali ikatokea.
Walisema
kuwa ni vema sasa Serikali ikachukua hatua kali kwa madereva wazembe
ili kuzinusuru roho za watu ambao ni nguvu kazi ya taifa ambazo
zinateketezwa kwa uzembe wa
madereva.
Hii inakuwa nia ajali ya pili ya mabasi ya abilia
kutokea katika barabara ya Musoma kwenda Mwanza ndani ya wiki mbili
baada ya kutokea ajali nyingine ya basi la Bunda Expless likitopkea
Wilayani Bunda kuelekea Mtukula.
Home
»
»Unlabelled
» WATU SABA WAFARIKI BAADA YA MABASI KUGONGANA USO KWA USO WILAYANI BUNDA
Post a Comment
0 comments