Musoma,
KUPANDA kwa
bei ya nyama mara kwa mara katika Manispaa ya Musoma kumepelekea
kuwatanisha viongozi wa Halmashauri ya Manispaa pamoja na Wafanyabiashara wa
nyama baada ya malalamiko kutoka kwa wananchi.
Katika kikao
hicho kilchofanyika katika ofisi ya Meya
wa Manispaa ya Musoma hoja ya
malalamiko ya Wananchi na kupelekea kikao
hicho ni bei ya nyama kutoka
shilingi elfu 4000 hadi 5000 ,huku bei
ya nyuma ikiwa kati y ash 2500
hadi 3000 kwa kilo ya nyama.
Zaidi ya
malalamiko ya Wananchi ni kutokana na madai ya kuwepo kwa idadi
kubwa ya ng’ombe katika Mkoa wa Mara tofauti na mikoa
mingine na badala yake bei imekuwa
ikipanda mara kwa mara na kuleta
kero .
Kwa upande
wao wafanyabiashara wa nyama katika manispaa ya musoma wamesema kuwa bei yao ni halali kutokana na
kupanda kwa ng’ombe katika minada kutokana na ushindani unaopatikana katika minada.
Mmoja wa
wafanyabiashara Joseph Magita amesema kuwa
wanunuzi wa ng’ombe minadani kutoka nchi jirani ya Kenya wamekuwa wakiharibu soko la ng’ombe minadani
kwa kupandisha bei ambapo inafika
wakati ng’ombe mmoja ananunuliwa hadi shilingi milioni moja na nusu.
‘’ Vipi
tutaendelea kufanya biashara ya hasara kwa maana zaidi ya milioni moja kwa
ng’ombe huwezi kununua na kuuza shilingi
elfu 3000 kwa kilo lazima tuangalie kipindi cha soko
‘’alisema Magita.
Hata hivyo
hoja za wafanyabiashara hao kuhusiana na
ushindani wa bei minadani zilikinzana na
viongozi pamoja na madiwani waliokuwepo
katika kikao hicho kwa madai soko la
nyama katika wilaya nyingine za mkoa wa mara ambao wananunua
katika soko moja na ipo chini.
Diwani wa Kata ya Makoko (CHADEMA) na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Aloyce Mawazo alisema wafanyabiashara wa nyama
katika Manispaa ya Musoma lazima
waliangalie suala la bei ili kuendana na soko la ulaji
wa nyama.
Kwa
upande wake Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura (CHADEMA)
aliwashauri wafanyabiashara hao kuto kuangalia kutaka faida kubwa katika
biashara bali waangalie mzunguko wa kibiashara ambao wanaufanya katika
soko kutokana na muitikio wa walaji.
Alisema
kwa sasa walaji wengi wameshindwa kununua nyama kutokana na kupanda kwa
bei hali inayosababisha kulala kwa nyama katika mabucha kwa zaidi ya
siku mbili na kuwakosesha mapato.
"Natambua
mpo
katika soko hulia lakini lazima muungalie mzunguko wa kibiashara wa
nyuma na kipindi hiki ambacho mmepandisha bei...watu wengi hawanunui
nyama na sindhani kama itakuwa na faida kwenu na tumewaita hapa kupeana
ushauri na sio kuwapangia bei,"alisema Kisurura.
Katika
hatua nyingine Meya huyo wa Manispaa ya Musoma amesema wapo katika
mabolesho makubwa katika machinjio ya nyama na bucha ili kuweka mahala
salama pa kuchinjia na kuuzia nyama.
Alisema
Manispaa ya Musoma imetenga shilingi milioni 9 zikilenga kufanya
ukarabati katika bucha za soko kuu la Musoma ikiwa ni pamoja na kuwekea
nishati ya umeme na ukarabati wa
jengo.
Post a Comment
0 comments