Na Shomari Binda
Musoma,
HOSPITALI ya
mkoa wa Mara iko katika hatari kubwa ya kukubwa na milipuko ya magonjwa
mbalimbali yakiwezo ya kuhara kutokana na wodi zake nyingi kukosa vyoo jambo
ambalo linasababisha wagonjwa kujistili
ovyo ndani na nje ya wodi hizo.
Mwandishi wa
habari hizi juzi alishuhudia kinyesi kingi kikiwa kimetapakaa nje ya wodi hizo
huku wagonjwa wakitumia vyombo kama madishi na majagi kwaajili ya kuhifadhia
mkojo.
Baadhi ya
watu ambao wanaguza ndugu zao katika wodi namba saba na tatu katika hospitali
hiyo,waliliambia gazeti hili kuwa wagonjwa wanalazimika kujisitili nje ya wodi
hizo na kusababisha kutapakaa ovyo kwa
kinyesi hicho.
Walisema
hivi sasa wanalazimika kununua vyombo kama madishi na majagi kwaajili ya kuhifadhi
mkojo wa waguzi wa wagonjwa na wagonjwa
hasa nyakati jambo ambalo walisema linaweza kusababisha milipuko mikubwa ya magonjwa endapo hatua za haraka
hazitachukuliwa kukabili hali hiyo.
“Wewe ona
uwanja wote huu umejaa kinyesi hayo madishi uliyaona humu ndani si kwamba
yamehifadhi maji bali ni mkojo kwani wodi hii na zingine zote hazina vyoo”alisema
mama mmoja juzi usiku wakati akizungumza naBLOG HII .
“Sehemu hii
ambayo unaona kuna marundo marundo ya mchanga hicho ni kinyesi kimefukiwa na
watu asbihi wanakaa katika maeneo haya hivi unategemea nini kama si magonjwa…kweli
sehemu ya afya kama hii hali inakuwa hivi je hapa tunajifunza nini sisi”alihoji
mzee Ramadhan Said.
Mganga
mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa wa Mara Dk Iragi Ngerageza akizungumzia suala hilo kwa njia ya simu alikiri wodi hizo kukosa vyoo kwa madai kuwa majengo hayo
ni ya muda mrefu na kwamba tayari mhandisi wa ujenzi wa mkoa ameombwa kuandaa
michoro mipya ya kuwezesha ujenzi wa mfumo mzima wa maji machafu na vyoo hivyo.
“Ni kweli
kabisa hayo unayouliza ndio yapo katika hospitali hii,kama unavyojua mimi ni
mgeni nimekuja juzi nilipokuta hali hii nilitishika sana sana hivyo ilinibidi
kumwite mhandisi wa mkoa kwaajili ya kuona hatua za haraka za kuchukua ikiwa ni
pamoja na kuandaa michoro ya kuwezesha kujenga mfumo mzima wa maji machafu na
vyoo hivyo kwani majengo haya ni ya muda mrefu”alisema mganga huyo mfawidhi.
Hata hivyo alisema
baada ya waziri wa Afya na Usatawi wa jamii kuteua wajumbe wa bodi ya
uendeshaji wa hospitali hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa kesho,itasadia kwa
kiasi kikubwa kutatua changamoto nyingi zinazoikabili hospitali hiyo hivi sasa.
Post a Comment
0 comments