0
KIKOSI CHA GHANA


Baada ya timu za kundi A kucheza mchezo wa pili kila moja,leo ni kindumbwendubwe cha kundi B.

Vinara wa kundi hilo Mali itakuwa ikipepetana na Ghana, huku miamba ya kutoka misitu ya kati ya Afrika, DR Congo wataonyeshana kazi na Niger.

Mpaka sasa Mali ndiyo inayoongoza kundi hili kwa kujikusanyia pointi tau baada ya kuilaza Niger katika mechi yao ya kwanza, huku Ghana na DR Congo zote zina pointi moja moja kila moja.

Mali ndio watakaoanza kuchachafyana na Ghana, huku mechi ya pili ikiwakutanisha DR Congo na Niger itakayokuwa ikiwania pointi tatu kwani ikipoteza katika mchezo huo tayari itakuwa imejichimbia kaburi, kutokana na kutokuwa na pointi hata moja.
Kikosi cha DRC

 Timu zote zina nafasi ya kusonga hatua ya robo fainali iwapo zitachanga vizuri karata zao.

Katika kundi A, Afrika Kusini inaongoza ikiwa na pointi nne na kufuatiwa na Cape Verde na Morocco zenye pointi mbili kila mmoja.
 
Afrika Kusini itakayopambana na Morocco itahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya robo fainali, huku Cape Verde, Morocco na Angola zote zikihitaji ushindi katika mechi zao za

Post a Comment