WANAJESHI WA MALI |
Jeshi la Mali limewaua “kiholela watu kadhaa” katika
harakati za kujaribu kuteka tena eneo la kaskazini lililoko chini ya
mamlaka ya wapiganaji wa Waisilamu.
Hii ni kwa mujibu wa kikundi cha
kutetea haki za binadamu.
Shirikisho la Kimataifa la Kutetea Haki za
Binadamu, FIDH, limesema kwamba watu kadhaa waliuwawa kwa ajili tu
walikuwa hawana vitambulisho.Madai mengine kuhusu mauaji ya kiholela pia yameripotiwa katika maeneo mengine ya magharibi na kati mwa nchi hiyo.
Habari zinazosema kwamba jeshi hilo, ambalo wengi wao ni Waafrika weusi kutoka kusini mwa nchi, wamekuwa wakiwalenga Waarabu na Watuareg kutoka kaskazini, jambo linaloashiria ubaguzi wa rangi katika mapigano hayo, ubaguzi ambao umefichwa na kuwepo kwa vikosi kutoka nchi za magharibi wanaopambana na wanamgambo Kiisilamu.
CHANZO bbc swahili
Post a Comment
0 comments