0
Takriban watu 8 wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mapigano mapya eneo la Tana River kusini mashariki mwa Kenya. 

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu ambalo limedai
Mamia waliuawa mwaka jana katika mapigano mengine ya kikabila katika eneo hilo.
Wawili kati ya watu wanane waliouawa wanaaminika kuwa washambuliaji walioshambulia kijiji cha Orma usiku wa kuamkia leo.

Watu wengine watatu walijeruhiwa vibaya , kwa kukatwa katwa na mapanga hali imekuwa ya wasiwasi huku kukiwa na tetesi za kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Polisi mmoja alithibitisha kuwa watu wanane waliuawa , tisa kujeruhiwa na kuwa nyumba ziliteketezwa wakati wa mashambulizi hayo.
 
Ghasia hizi mpya zimesababisha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama na uwezo wa polisi kuthibiti hali katika maeneo tete.
Katika eneo hilo ghasia zilizuka kwa mara ya kwanza mwezi Agosti mwaka jana ambapo watu wa jamii za Pokomo ambao ni wakulima walipigana na jirani zao wa Orma ambao ni Wafugaji na kusababisha mauaji.

Mwezi Disemba pekee watu 45 waliuawa katika shambulizi lengine.
Jamii hizo zimewahi kupigana na mzozo wao umekuwa ukisemekana kusababishwa na mgogoro wa maji na malisho ya wanyama.

Lakini kwa sababu ya hali ya mashambulizi yenyewe ambapo watoto na wanawake wamekuwa wakiuawa na nyumba kuteketezwa. 

Post a Comment