0
                                                          
Howard Webb ameteuliwa kusimamia mechi ya ligi kuu ya premier kati ya Manchester United na Liverpool katika uwanja wa Old Trafford, siku ya Jumamosi.

Refa huyo, ambaye alisimamia mechi ya fainali ya kombe la dunia mwaka wa 2010, hajasimamia mechi yoyote tangu
mechi ya FA iliyokumbwa na utata miaka miwili iliyopita.


Katika mechi hiyo ambayo Liverpool ilishindwa kwa bao moja kwa bila katika uwanja wa Old Trafford, Webb aliipa Manchester United penalti na wakati huo huo kuumpa naodha wa Liverpool Steve Gerrad kadi nyekundu.

Mcheza kiungo wa Liverpool Ryan Babel, alipigwa faina na FA baada ya kuchapisha picha kwenye mtandao wa Internet unaomuonyesha Webb akiwa na jeshi la Manchester United.

Mwaka wa 2010 Webb, aliandikisha historia ya kuwa mtu wa kwanza kuwahi kusimamia mechi ya fainali ya kombe la dunia na pia fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya, katika kipindi cha mwaka mmoja.

Refa huyo mwenye umri wa miaka 41, amesimamia mechi za ligi kuu ya premier kila msimu tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2003.

Post a Comment