0


Madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wa mjini Musoma wamechoma nyumba na kuiteketeza kwa kile walichodai mmiliki wa nyumba hiyo alishiriki kumuua bodaboda mwenzao na kisha kumtumbukiza katika mto na kupelekea mauti yake.

Tukio la kuchomwa moto kwa nyumba hiyo ya Koti magere mkazi wa Kijiji cha Etaro lilitokea tarehe 7 ya mwezi wa pili majira ya mchana bada ya bodaboda hao kutoka maeneo ya Nyakato anapoishi mwenzao aliyeuwawa hadi katika Kijiji hicho kilichopo katika Wilaya ya Butiama na kisha kuichoma nyumba hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma alisema mwendesha pikipiki huyo aliyefahamika kwa jina la Magere Mugeta aliuwawa na watu waliojichukulia sheria  mikononi  baada ya kudai kuwa marehemu kabla ya tukio la kuuwawa mnamo tarehe 4 mwezi wa pili katika Kijiji cha Nyegina alimgonga mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Majani na kisha kukimbia akidhani kuwa ameua.

Alisema Wananchi wa eneo hilo walimkimbiza na kisha kumshambulia kwa siraha za jadi hadi kufa na kisha kumtumbukiza katika ndani ya mto ujulikanao kwa jina la Masimbi wenye kina zinazokadiliwa kufika futi tatu na kuibuka tarehe 7 na kuonwa na Wananchi ambao walitoa taarifa Polisi.

Kamanda Mwakyoma alisema pikipiki aliyokuwa akiitumia marehemu huyo yenye namba T 509 BCE ilikutwa nyumbani kwa balozi wa eneo hilo aiitwaye Alex Nyarukamo  (61)Mkazi wa Etaro Masimbi ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Katika tukio lingine Kamanda Mwakyoma alisema mtu mmoja aitwaye Rhobi Marwa (32) mkazi wa Nyamakendo aliuwawa kwa kukatwa mapanga sehemu za shingoni,shavu la kushoto na mkono wa kushoto na mtu aitwaye Mwita Wambura (28).

Mwakyoma alisema tukio hilo lilitoke afebruari 7 majira ya saa 11 jioni katika Kijiji cha Nyamakendo kata ya Machonchwe Wilayani Serengeti ambapo alidai uchunguzi wa awali kuhusiana na tukio hili ulibaini chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi na mtuhumiwa amekatwa huku taratibu za kumfikisha mahakamani zikifanywa.

Kutokana na matukio hayo kamanda Mwakyoma ameendelea kutoa wito kwa Wananchi na madfereva wa pikipiki wa kubeba abiria maarufu kama bodaboda watii sheria za Nchi bila kushurutishwa na kuepuka kujichukulia sheria mikononi kwani kuendelea kufanya hivyo ni kuvunja sheria za Nchi

 Alisema tayari kuna watu ambao wameshachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kutokana na kujichukulia sheria mikononi na hivyo kuwataka Wananchi ambao bado wanaendelea kuto tii sheria endapo watakamtwa kutokana na kujichukulia sheria mikononi watafikishwa katika vyombo vinavyohusika.

Post a Comment