0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Manispaa ya Musoma 
kimeendelea kuwa na kutokuelewana ndani kwa ndani ambapo kesho wanatarajia kufanya kikao kwa
ajili ya kumjadili Diwani wa kuteuliwa   Habiba Ally kwa
madai kuwa amekuwa akipingana na hoja ya Chama hicho.

Habari ambazo BLOG HII imepata tetesi zake   zinadai Diwani
huyo wa amekuwa hawaungi mkono katika hoja mbalimbali ndani
ya chama hicho na katika vikao mbalimbali vya Baraza la Madiwani.

Mmoja wa madiwani wa Chama hicho ambaye hakutaka kutaja jina lake
alisema kesho hii kuna kikao cha kawaida ingawa hajui nini
kitazungumzwa au kuna maamuzi gani yatakayojadiliwa. 

“Kesho tunatarajia kuwa na kikao cha kawaida cha Chama lakini sina uhakika
kama kuna ajenda hiyo ya kujadiliwa kwa Diwani huyo nadhani baada ya kikao utafahamu zaidi kutoka kwa viongozi kitakachoongelewa,"alisema 


Alidai Diwani huyo ni mtu mzima hivyo hawezi kuunga mkono jambo
ambalo anaona wazi kuwa anaburuzwa lazima jambo la muhimu ambalo
wanatakiwa uongozi kujua ni pamoja na kumuita na kumhoji na hatua ziende
ngazi za juu na kujadiliwa kisha maamuzi yatafanywa kupitia viongozi kwa ajili ya hatua zaidi. 

“Kila mtu ana maamuzi yake binafsi huwezi kuunga mkono mambo ya
kijinga jinga na kama watafanya hivyo hiyo itakuwa sio Demokrasia bali
ni udikteta ndani ya chama,”aliongeza.

 Binda News na Blog hii lilifanya jitihada za kumtafuta Diwani anayedaiwa kutaka kujadiliwa katika kikao cha kesho Habiba Ally ili kutaka kujua kama anazo taarifa juu ya kikao hicho hakuweza kupatikana na hata walipotafutwa viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Musoma nao hawakuweza kupatikana.  

Ndani ya Chama hicho hivi karibuni  wameonekana kutaka kuwekana sawa
ambapo madiwani wa Chama hicho pamoja na wa Vyama vingine vya CUF NA CCM  waliitisha kikao dharura cha Baraza la
Madiwani Februari 16 mwaka huu kwa ajili ya kutaka
kumng’oa Meya wa Manispaa hiyo Alex Kisurura kwa kile walichokieleza kusaini Bajeti bila kujadiliwa na madiwani.

Katika kikao hicho Mkurugenzi Ahmed Sawa alinusuru hali hiyo baada ya
kutoa maelezo ya kina kuwa katika kuandaa bajeti hiyo Meya huyo
alikuwa safarini Dar es salaam na chanzo cha kupeleka bajeti hiyo bila
kufuata taratibu ni kutokana na mabadiliko ya Bunge la bajeti ndipo
madiwani hao waliposhusha jazba zao.

Kikao hicho kilihoji kwa nini Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2013/14 ilifika
Wizara ya Fedha bila kufuata taratibu za vikao vya kamati mbalimbali
  kisha kikao cha baraza kwa ajli ya
Maamuzi.

Post a Comment