1
MFANYAKAZI wa ndani aliyejulikana kwa jina la Sabina Dominick (21)
Mkazi wa Biharamulo Mkoa wa Kagera aliyekuwa anafanya kazi Manispaa ya
Musoma Mkoa wa Mara ameuawa kwa kunyongwa na kipande cha pazia na
Magesa Mathias ambaye baada ya kutekeleza mauaji hao naye alijinyonga.

Tukio hilo lililotokea Februari 19 mwaka huu saa 12 jioni katika mtaa
wa Kawawa nyumba namba 35 inayomilikiwa na Magori Chacha
mfanyabiashara wa mafuta Mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom
Mwakyoma alisema kuwa mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa mikono na
miguu kamba iliyotumika kumnyongea ilikuwa shingoni.

“Kabla ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa ambaye naye alijinyonga
kwa kutumia kamba ya manira kwa kujitundika kwenye chuma kinachobeba
tanki la maji aina ya Simtank alimjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni
Mugesi Magori (21) ambaye ni mke wa Magori,”alisema Kamanda Mwakyoma.

Majeruhi huyo amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa huo kwa matibabu zaidi
ambacho chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na uchunguzi wa kina
unafanyika ili kuepusha maafa zaidi.

Katika tukio lingine,Kamanda Mwakyoma alisema kuwa Jeshi hilo linamshikilia Mwikwabe
Marumbe mtuhumiwa wa mauaji wa tukio lilitokea Februari 11, mwaka huu
saa 1:30 asubuhi
maeneo ya Kijiji cha Mkirira wilaya ya Butiama.  


Mwanamke aliyejulikana
kwa jina la Ziada Sasita (35) mkazi wa kijiji cha Kabegi aliuawa kwa
kunyongwa shingo yake kwa kutumia nguo yake mtandio hadi kufa na watu
wasiojulikana.

Marehemu alikuwa anatokea kwa mjomba wake maeneo ya mkirira ambako
alikuwa ameenda kumsalimia na siku ya tukio alikuwa anarudi kabegi
ambako alikuwa ameolewa. 


Mwili wa marehemu ulikutwa na mtandio
shingoni na ulimi wake ukiwa umetoka nje.

Post a Comment

this link tramadol medication purchase - buy tramadol tennessee