1








Wakazi wa maeneo mbalimbali ya Manispaa ya musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla wameendelea kutoa hoja zao katika kipindi cha Mini Buzz kinachorushwa na TBC1 zikiwa ni hoja za mada mballimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kuanzia siku ya jumatatu ya wiki hii walipoingia mjini Musoma.

Wananchi hao wameonekana kutokuwa na woga katika kutoa hoja zao katika mada zinazotolewa hali iliyopelekea waendeshaji wa kipindi hicho kufurahia jinsi wakazi wa mji wa mussoma walivyo tayari kutoa hoja zao.

Kesho alhamisi timu inayoendesha kipindi hicho itaelekea Wilayani Tarime ili wananchi wa huko wapate kutoa hoja zao na kusikikaka sehemu mbalimbali ambapo TBC1 inapatikana.

Post a Comment

Kazi njema Shommy & Min Buzz Anchors wote.
Ni wakati muafaka kufikiria namna mawazo chanya ya kimaendeleo yanayotolewa katika vipindi kama hivi vya ndani ya Min-Buzz kufanyiwa mkakati makusudi wa kukusanywa, kuyafanyia muhtasari na kuyasambaza katika vyombo mbalimbali vya Serikali na Asasi zisizo za kiserikali kama michango mwanana wakati wa Watz wanabangua bongo kushiriki katika kujiletea maendeleo yao wenyewe katika nyanja mbalimbali. Wengine wanaweza ona kuwa hili ni jambo dogo hivi kama la kuburudisha tu. La hasha, maendeleo yeyote yanakuja kwa wananchi kuwa tayari kutafakari maisha yetu na kujadiliana kwa heshima na uwazi namna tunavyoweza kuboresha maisha yetu na kuendeleza nchi yetu wenyewe kwa kumsikiliza kila mtu si tu viongozi bali wananchi wote popote hata wakiwa barabarani!Ukinishusha mimi, Min- Buzz iendelee na mada ya leo!!!