0
DIWANI wa kata ya Sabasaba iliyopo Wilayani Tarime Christopher Chomete (CHADEMA) amemjia juu Mbunge wa Jimbo la Tarime Nyabali Nyangwine (CCM) kwa kile alichodai kuahidi katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kuwa kipaumbele chake mara atakapochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ni kuhakikisha maji yanatoka katika ziwa victoria na kusambazwa katika Wilaya hiyo kiti ambacho amekikalia kimya.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halimashauri ya Wilaya hiyo,Chomete alisema katika kipindi cha kampeni Mbunge huyo kila katika mkutano wake wa kampeni alikuwa akisisitiza kipaumbele chake kikubwa kitakuwa huduma ya maji safi kwa Wananchi wa Wilaya ya Tarime lakini hadi leo hakuna dalili yote inayoonyeshwa na Mbunge huyo katika kulifanyia ufumbuzi suala la huduma ya maji huku Wananchi wakiendelea kupata hadha kubwa ya maji katika Jimbo hilo.

Alisema Wilaya ya Tarime kwa sasa imeendelea kuwa na ongezeko kubwa la watu wanaofanya bishara mbalimbali na wafanyakazi wa kada mbalimbali lakini tatizo la maji limekuwa ni kero kubwa huku asilimia kubwa ikitumia maji yanayotokana na visima licha ya Wilaya hiyo kuwa karibu ziwa victoria.

Chomete alisema ameamua kulizungumzia suala hilo katika kikao cha Baraza la madiwani kutokana na ukimya wa Mbunge huyo licha ya kuahidi kulifanyia kazi suala la maji katika kipindi kifupi atakapokuwa Mbunge wa Jimbo hilo ili Halimashauri ione namna ambavyo inaweza kufanya utaratibu mwingine wa kufanya mchakato wa kuhakikisha kero ya maji kwa Wananchi wa Tarime inafanyiwa kazi.

Alisema hajawahi kumsikia Mbunge Nyangwine akisimama katika Bunge na kuzungumzia tatizo la maji katika Wilaya hiyo wala kuhitisha mkutano na kuwaeleza Wananchi kama kuna jitihada zozote ambazo amekwisha anza nazo kufika katika Wizara ya Maji na hivyo kupata wasiwasi na maenono ya Mbunge huyo aliyokuwa akityatoa katika kampeni kuwa alikuwa akiwadanganya Wananchi wa Tarime.

"Suala la Maji linamgusa kila Wananchi wa Wilaya ya Tarime kutokana na umuhimu wake,Mbunge Nyangwine kulikuwa hakuna mkutano wa kampeni mbao alikuwa akisimama na kushindwa kuzungumzia suala la kero ya Maji kwa Wilaya ya Tarime sasa ukimya ambao ameuonyesha kwa kipindi hiki lazima tumkumbushe.

"Alisema kwenye mikutano suala la Maji lingekuwa kipaumbele chake mara baada ya kuchaguliwa lakini hadi leo hakuna taarifa zozote kuwa suala hilo limefikia wapi huku tatizo la Maji likiendelea kuwa kubwa katika Wilaya ya Tarime,"alisema Diwani huyo.

Kabla ya kuendelea kuzungumzia sula hilo la Maji,Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime Athumani Akalama alimtaka Diwani huyo kutolizungumzia sula hilo bali atafute mahala ambapo anaweza kulizumzia lakini katika Baraza hilo sio mahala pake.

Kauli hiyo ilimfanya Diwani Chomete kuja juu nakumueleza Mkurugenzi huyo kuwa azisome kanuni ili azielewe vizuri kwani Mbunge kwa mujibu wa kanuni ni Diwani wa Baraza hilo anapokuwepo na yeye kulielezea sula hilo yupo sahihi kwa mujibu wa kanuni.

Post a Comment