Mamia ya Wakenya wamehudhuria mkusanyiko wa mwisho wa sala mjini Nairobi, kuomba uchaguzi mkuu wa juma lijalo uwe wa salama.
Mhadhara huo wa ibada umefanywa baada ya polisi kusema kuwa vipeperushi vinavochochea fujo vilisambazwa katika baadhi ya maeneo. Wagombea kadha wa urais walihudhuria mhadhara huio pamoja na Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta. Uhuru Anakabiliwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu
kuhusu ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa Kenya miaka mitano
iliyopita ambazo ziliuwa watu zaidi ya elfu moja.
Post a Comment
0 comments