0
WILAYA ya Butiama mkoani Mara imeelezwa kuwa miongoni mwa Wilaya 26 Nchini zisizokuwa na Mahakama ya Wilaya hivyo kuwa kichocheo cha watu kijichukulia Sheria mkononi.

Hayo yamebainishwa leo kwenye mkutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kilichofanyika katika ukumbi wa Uwekezaji uliopo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa mara,mjini  hapa.

Akiwasilisha Taarifa ya kamati ya maadili ya Wilaya ya Butiama,Mwenyekiti wa kamati hiyo ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma,Angellina Mabula alisema mbali ya wilaya yake kukosa mahakama ya wilaya  kati ya mahakama 7 za mwanzo ni 2 tu zenye uwezo wa kufanayakazi kutokana na zingine kuwa na miundo mbinu chakavu huku zikikosa Mahakimu.

Alifafanua kuwa pamoja na Mahakama hizo kuwa na uwezo wa kutumika hakuna Hakimu hata mmoja,ambapo makarani waliopo ni wawili kukiwa hakuna mpigachapa hata mmoja''kwa mapungufu haya dhana ya upatikanaji wa haki kwa wakati haiwezi kufikiwa katika wilaya ya Butiama na ndio maana kunakuwa na matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi''alisema

Awali Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othumani Chande ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama alisema pamoja na kuwa kisheria kila Wiolaya inapaswa kuwa na mahakama bado kuna Wilaya 26 ambazo hazina Mahakama za Wilaya huku Mikoa 12 ikiwa haina Mahakama za Mkoa.

Aliosema mbali na changamoto hizo Mahakama haina budi kutimiza wajibu wake kwa dhamila ya kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati kwani mbali na kulinda Katiba Mahakama inajukumu la kutoa huduma ya haki kwa Wananchi"Kesi zisikae Mahakamani kwa zaidi ya miaka miwili"alisisitiza.

Akitoa ufafanuzi kuhusu lengo la ziara hiyo,Jaji Mkuu alisema pamoja na tume hiyo kuwa katika muundo mpya lengo ha;lisi ni kukutana nma kamati za maadili za Wilaya na Mikoa kwa ajilio ya kubadilishana m,awazo kiutendaji.

Alifafanua kuwa maamuzi yeyote hayawezi kutolewa na tume yake bila kupata ushauri na maoni kutoka katika kamati hizo hivyo ipo haja ya kutafuta njia na namna ya kuziimalisha ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Jaji Chande alisisitiza kuwa katika muundo huo mpya bajeti ya Mahakama kwa sasa itatoka katika mfuko wa Mahakama anbapo wafanyakazi wote wa Mahakama Nchini wapatao 6238 watakuwa chini ya Tuime badala ya kuwa chini ya Mamlaka ya Utumishi kama ilivyokuwa hapo awali.

Akiongelea mafaniko ya Tume hiyo tangu ilipoanza utaratibu wa kazi,mbali ya kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa watendaji wakuu wa Mahakama kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kuajiri Mahakimu wenye Digrii yta Sheria katika Mahakama za mwanzo.

Akizungumza katika kikao hicho ambacho pia kiliwashirikisha wajumbe wa Kamati za maadili kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara,Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya MaadiliI ya Mkoa alisema Tume hiyo imekuja katika wakati muafaka kwani itawafungua zaidi kiutendaji na kufanya kazi kazi kwa kuziongatia weledi.

Alisema Wananchi wanategemea sana Mahakama katika upatikanaji wa Haki hivyo kuna wajibu katika Tume za Maadili kufanya kazi kwa kuzingatia haki ili maamuzi yanapotolewa kutoka katika Tume ya Maadili kila upande uweze kulidhika na maamuzi yatakayotolewa.

Post a Comment