0


 Wanajeshi wa jeshi la wanamaji la Marekani, wamekubali mashtaka ya kumbaka mwanamke mmoja katika kesi ambayo imeibua hisia kali dhidi ya Marekani.

Wanaume hao. Walimvamia mwanamke huyo wakati wa ziara yao fupi katika kisiwa cha Okinawa, makao kwa kambi kubwa ya jeshi la Marekani barani Asia.

Sheria ya kutotoka nje iliyowekewa wanajeshi karibu elfu hamsini kufuatia tukio hilo Okotoba mwaka jana
Kumekuwa na hali ya wasiwasi kati ya majeshi ya Marekani na wenyeji wa Okinawa.

Manamo mwaka 1995, genge la wanajeshi wa Ulaya, lilimvamia na kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12 na kuzua maandamano makubwa.

   chanzo BBC NEWS

Post a Comment